26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Unyanyapaa, tabia hatarishi bado ni mwiba mapambano VVU

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

UNYANYAPAA na ubaguzi umetajwa kuwa bado ni kikwazo katika mapembano dhidi ya UKIMWI nchini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni kwenye Warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Maofisa Habari na Waratibu wa Ukimwi wa Mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani iliyofanyika mjini Bagamoyo kwa kuratibiwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake na Usawa wa Kijinsia (UN WOMEN).

Mwezeshaji kutoka shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wanawake na uhamasishaji wa usawa wa jinsia –UN WOMEN,  Jakob Kayombo 

Akizungumzia mafunzo hayo, Afisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Innocent Byarugaba, amesema mafunzo hayo yamemjenga kujua kwanza mila potofu, haki za binadamu na kuondokana na upofu uliko katika jamii katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

“Mafunzo haya kwanza yamekuja kwa wakati kwani tunakwenda kuibadilisha jamii kutoka kwenye upofu wa masuala ya VVU kwenda kwenye uelewa.

“Hivyo tunakwenda kufanya kazi kwenye mkoa wetu wa Pwani ikiwa ni pamoja na kujiwekea mkakati maalumu ili kufundisha jamii yetu iweze kubadilika.

“Kwani ni wazi kwmaba katika mkoa wetu bado kuna mambpo ambayo hayatii faraja sana kama binadamu, kwani bado kuna watu wanaojiuza, wanaobakwa, watoto wanaonyanyaswa pia tuna mimba za utotoni.

“Hivyo kazi yetu ni kwenda kuwabadilisha hasa wanaotekeleza mambo haya waelewe na wao, wawe sehemu ya kuibadilisha jamii na kutambua kuwa mambo haya hayafai na pengine tunawapotezea ndoto watoto ambao wana maelengo mengi makubwa ya kutaka kulitumikia taifa lao,” amesema Byarugaba.

Upande wake, Dk. John Sijaona kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, amesema mila hatarishi ni sababu ambayo imeendelea kuchochea maambukizi ya VVU katika mikoa ya Kusini.

“Wanajamii wamekuwa wakichukulia tofauti suala la jando na unyago kwani changamoto imekuwa ikijitokeza siku wanayotolewa watoto. Kwani baadhi ya wanaotoka kwenye mafunzo hayo ya unyago wamekuwa wakiona kuwa sasa wanayo fursa ya kufanya kila kitu hatua ambayo imekuwa ikichochea maambukiz.

“Pia katika jando wakati mwingine wale mangariba wamekuwa hawazingatii usafi wa utakasaji wa vifaa vyao kwani unakuta muda mwingine wanatumia kifaa kimoja kwa vijana zaidi ya watatu hatua ambayo inachochea maambukizi,

“Hivyo tumejengewa uwezo ambao tunaamini kuwa tutaendakuutumia katika kupambana na mila na desturi kwenye kupunguza maambukizi ya VVU,” amesema Dk. Sijaona.

Nae Mwajina Lipinga, ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Ofisi ya Rais-(TAMISEMI) na Mratibu wa Jinsia na Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, amesema lengo ni kwajengea uwezo wataalamu mbalimbali ili waweze kuishirikisha jamii kuweza kuchangia kwenye utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayoweza kiupunguza madhara kwenye jamii.

“Mafunzo haya yanayotolewa yanalenga kuona ni kwa namna gani watalaamu hawa katika serikali za mitaa watakavyoweza kushiriki na kushirikisha jamii katika kuchangia utekelezaji wa mikakati mbalimbali ambayo tunafikiri kuwa inaweza ikasaidia kupunguza mila na desturi ambazo zinaleta madhara kwenye jamii ikiwamo kuongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.

“Matumaini ya serikali katika kuwajengea uwezo wataalamu hawa kutasaidia kuwafanya kuwa chachu katika kutekeleza majukumu yao kutegemeana na taaluma mbalimbali.

“Hii itasaidia kuhakikisha kwamba kwenye Halmashauri ambako ndiko kwenye kiini cha utekelezaji wa mipango hii kutawezesha jamii kupata uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Ukimwi pia mila na desturi za kijinsia ambazo kwa namna moja au nyingine zinachangia kuongeza kasi ya maambukizi ya Ukimwi hasa kwa wanawake na watoto wa kike,” amesema Mwajina.

Akizungumzia changamoto kubwa iliyoko katika mapambano dhidi ya VVU, amesema kuwa ni mila na desturi.

“Changamoto ni nyingi lakini ambayo iko wazi ni ile ya mila na desturi ambazo jamii imekuwa nazo kwa muda mrefu, hivyo suala la kumuachanisha binadamu na mila hizo siyo suala la siku moja.

“Hivyo, hata elimu hii inayotolewa haiwezi kutolewa kwa siku moja tukasema tumemaliza inatakiwa iwe endelevu, lengo kubwa ni kubadilisha mitazamo na fikra ilizonazo jamii kuhusu masuala ya mila na desturi ambazo zinachangia maambukizi ya VVU,” amesema Mwajina.

Akizungumza mara baada ya warsha hiyo, Afisa Jinsia kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Judith Luande, amesema lengo la kukutana na makundi hayo ni kuwajengea uwezo kwa kuwa ndio watu waratibu muhimu wa shughuli za ukimwi kwneye maeneo yao.

“Kama tunavyofahamu kwamba Maafisa Habari na Waratibu wa ukimwi kwenye mikoa na halmashauri kw aujumla ni watu muhimu katika kutekeleza mapambano haya dhidi ya Ukimwi.

“Hivyo tunaamini na kutambua kwamba iwapo watajengewa uwezo basi itakuwa ni rahisi katika kuifikia jamii kwani ikiwamo kubadilisha mtazamo na mila zinazochochea maambukiz ya VVU,” amesema Judith.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles