25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

United waweka historia ya miaka 31

MANCHESTER, ENGLAND

TIMU ya Manchester United, imeandika historia mpya msimu huu ya kufanya vibaya ambapo haijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka 31 kwenye Ligi Kuu England.

Mwishoni mwa wiki iliopita timu hiyo ilikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Old Trafford na kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Aston Villa na kuufanya kuwa mchezo wa sita msimu huu kwenye michuano hii kutoka sare.

Mbali na kutoka sare kwa michezo sita, lakini imekubali kichapo cha michezo minne na kushinda michezo minne katika michezo 14 waliocheza msimu huu.

Hii haijawahi kutokea kwa timu hiyo katika historia yake tangu msimu wa 1988-89 wakiwa wamecheza michezo kama hiyo. Sasa Manchester United imeachwa kwa pointi 22 dhidi ya vinara wa Ligi hiyo Liverpool.

Msimu huo wa mwaka 1988, Manchester United walimaliza nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi huku wakiachwa kwa pointi 25 dhidi ya Arsenal ambao walikuwa mabingwa, lakini ubingwa huo ulitokana na idadi kubwa ya mabao baada ya kuwa sawa kwa pointi na Liverpool.

United msimu huu imekuwa kwenye wakati mgumu chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, hivyo kocha huyo yupo hatarini kufungashiwa virago.

Mbali na kufanya usajili wakati wa kiangazi bado United inaonekana inakosa muunganiko kuanzia safu ya ulinzi, kiungo pamoja na ushambuliaji, lakini beki wa kati wa timu Harry Maguire amedai bado wanapambana kuhakikisha wanakaa vizuri, ila kwa sasa bado timu haiko sawa.

“Tunajitahidi kupambana ili kuwa bora zaidi kwa kuwa ushindani ni mkubwa na bado hatupo sawa, kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani ni kitu cha kuumiza mashabiki na timu kwa ujumla,” alisema mchezaji huyo.

Kwa upande mwingine wiki hii ni ngumu kwa Man United ambapo kesho watakuwa nyumbani kupambana na Tottenham ikiwa na kocha wao mpya Jose Mourinho, huku mwishoni mwa wiki Jumamosi watakutana na majirani zao Man City kwenye Uwanja wa Etihad.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles