20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

UNESCO YATANGAZA MAENEO MAPYA YA KIHISTORIA DUNIANI


Shirika la utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO limetangaza maeneo mapya ya kihistoria duniani kote.
Kwa mujibu wa UNESCO, kuorodheshwa katika orodha hiyo kuna yapa maeneo hayo ulinzi wa kisheria chini ya mikataba ya kimataifa, UNESCO imesema.
Maeneo yaliyotajwa ni pamoja na Thimlich Ohinga ni ukuta mkubwa zaidi wa makazi ulio jengwa kwa mawe katika kanda ya ziwa Victoria Kenya.
Pia katika Mashariki ya Omani, mji wa Qalhat ilikuwa ni bandari kubwa katika karne ya 11 na 15. Hii ni shuhuda kubwa ya akiolojia kwani ndio kiungo kati ya mashariki mwa Saud Arabia na Dunia kwa ujumla.
Nalo eneo lenye vijiji 10 linalopatikana katika kisiwa cha Kyushu, kuna ngome na kanisa kuu na yalijengwa katika karne ya 18 na 19, wakati ambapo imani ya Kikristo ilipigwa marufuku nchini Japan.
Bila kusahau jiji la Mumbai ambapo tangu imekuwa kitovu cha biashara ya kimataifa mwishoni mwa karne ya 19, Mumbai ili jiingiza katika mradi wa mpango miji, kujenga majengo mazuri kwa matumizi ya makazi na biashara.
Eneo linguine ni Al-Ahsa, katika Rasi ya Uarabuni Mashariki, ni bonde kubwa zaidi duniani na limekuwa nyumbani kwa binadamu kutoka zama za Waneolithiki hadi sasa.
Pia katika eneo hili kuna miti ya minazi milioni 2.5, bustani, mifereji, chemchemi, visima, ziwa lililo kauka, mifereji ya maji, majengo ya kihistoria na maeneo ya akiolojia.
UNESCO inapatazama hapa kama mfano pekee wa mahusiano ya binadamu na mazingira”
Imetajwa pia milima Sansa iliyopo eneo la kusini mwa Korea Kusini, imekuwa ukiendeshwa kama vituo vya imani tangu karne ya 7. Mahekalu hayo saba yana viwanja vya wazi na kumbi za mihadhara.
UNESCO inayaita maeneo haya kuwa ni maeneo matakatifu ambayo yame himili kuwepo kama kituo cha ibada na sehemu ya kila siku katika maisha ya kidini mpaka sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,102FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles