25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UNECA: Tanzania isiagize bidhaa nje

10569991454_30d97b3fae_bNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

OFISA wa Umoja wa Mataifa Kitengo cha Uchumi Afrika (UNECA), Hopestone Chavula, ameishauri Tanzania kuzalisha bidhaa zenye viwango ili kukwepa kuagiza vitu kutoka nje ya nchi.

Ushauri huo ameutoa jijini hapa jana wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa maendeleo ya viwanda na biashara Afrika kwa mwaka huu iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar es Salaam Convention Center.

Chavula alisema watu wengi wamekuwa wakiamini bidhaa zenye ubora ni zile zinazozalishwa nje ya nchi, hivyo kuzidi kudidimiza uuzwaji wa malighafi za ndani jambo linalochangia viwanda kuzidi kufa.

“Licha ya kubaini kuwa yapo mambo mbalimbali yanayochangia kushuka kwa hali ya biashara na viwanda nchini, kubwa ikiwa ni ukosefu wa miundombinu bora kama barabara, umeme na maji, lakini bidhaa nyingi kuingia kutoka nje ndio kumechangia zaidi,” alisema Chavula.

Alisema ripoti hiyo imebaini kuwa endapo wakulima watazalisha mazao mengi kwa kiwango kizuri na wafanyabiashara wakaongezea thamani ya malighafi zao huku Serikali ikifufua viwanda, kutasaidia kukuza biashara na kuliingizia taifa pato kwa kuuza bidhaa nje ya nchi.

Alisema taifa litafikia wakati ambao litaacha kutumia vitu kutoka nje. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini (CTI), Samuel Nyantahe, alisema maendeleo yanategemea viwanda lakini kwa sasa nchi
imevamiwa na bidhaa za nje hivyo inapaswa kufufua viwanda vilivyopo.

Alisema viwanda hivyo ni pamoja na vinavyoshughulikia kilimo, uchimbaji wa madini na zana nyingine na kuongeza ubora wa bidhaa.

“Lakini mpango huu ili ufanikiwe inabidi wafanyabiashara na wenye viwanda kuungana kutatua tatizo na ndilo lengo la ripoti hii,” alisema Nyantahe.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu waWizara ya Afrika Mashariki, Joyce Mapunjo, alisema Serikali ipo kwenye mkakati wa kuandaa mpango wa miaka mitano ambao utaweka mkazo kwenye sekta ya viwanda na kuvifufua.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles