27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

UNAKUMBUKA UCHURO WA NDOA YA MAMA NA MWANA? HATIMAYE WAMETALIKIANA BAADA YA KUISHI ZAIDI YA MIAKA 8

NI simulizi ya kushangaza iliyoibuka mara ya kwanza mwaka 2012, lakini ambayo inaendelea kuzunguka mitandaoni kiasi kwamba, wale ambao hawakukisikia wanadhani ni tukio la juzi.

Inawahusu Betty Mbereko, mjane kutoka Kijiji cha Mwenezi huko Masvingo, nchini Zimbabwe kuwa na uhusiano wa kindoa na mtoto wake wa kumzaa Farai Mbereko.

Hata hivyo, taarifa mpya zinasema wawili wametalikiana nchini Afrika Kusini walikokimbilia.

Wakati wa enzi zao, si tu kwamba mama na mwanae, kila mmoja alikiri kuchizika na penzi la mwenzake, bali pia walikuwa wakitarajia kupata mtoto kwa vile mjane huyo alikuwa na mimba ya miezi sita iliyotokana na uhusiano wao huo haramu, japokuwa halali kwa mtazamo wao wenyewe!.

Mbali ya ujauzito huo, ambao Betty alitarajia kumzalia mwanae mtoto, ambaye kwa maneno mengine mjukuu wake, wawili hao walipanga kukata mzizi wa fitina kwa kuelekea altareni kufunga ndoa, kitu ambacho walikitimiza.

 

Baadaye wawili hao wakawa hawajulikani waliko baada ya kukikimbia kijiji walichokuwa wakiishi na kwenda kusikojulikana baada ya kugoma kuvunja ndoa yao hiyo.

Wakati ikijulikana kuwa si kosa kuoa au kuolewa na ndugu wa karibu bila kujumuisha ndugu wa damu kama kaka na dada au mzazi na mwana katika baadhi ya nchi na tamaduni nyingi duniani, nchini Zimbabwe uhusiano wa aina hiyo bila kujali aina ya udugu unahesabiwa kuwa uchafu.

Wazee wa kijiji, ambacho familia hiyo iliishi, walieeleza masikitiko yako kwa tukio hilo kutokea kipindi hiki cha maisha yao badala ya miongo michache iliyopita.

Walisema laiti kama lingetokea kipindi cha nyuma, wangeichinjilia mbali familia hiyo kwa kuwaletea aibu na fedheha kubwa katika jamii yao.

Kwa mujibu wa mtandao wa jadeafrican.com, wenzi hao uhusiano wao ulipoanikwa hadharani mwaka 2012 ulikuwa tayari na umri wa miaka mitatu.

Mbereko, amekuwa mjane kipindi cha miaka 12 na amekuwa akiishi na mwanae huyo.

Alithibitisha kuwa kutokana na mimba yake ya miezi sita, aliamua kufunga ndoa na mwanae huyo kwa sababu hataki kurithiwa ndoa na ndugu wa marehemu mume wake.

Anasema kuwa mashemeji zake wamekuwa wakimghasi mara kwa mara wakitaka kumuoa, kitu ambacho alisema hakuwa tayari nacho.

Hayo yalifahamika wakati alipoishtua mahakama ya kijiji wakati alipoeleza bila aibu kuwa uhusiano wao ulianza miaka mitatu kabla.

Alisema baada ya kutumia fedha nyingi kumpeleka mwanae Farai shuleni kufuatia kifo cha mumewe, alihisi ana haki kabisa ya kufaidi matunda yaliyotokana na fedha zake hizo.

Anasema hakuna mwanamke mwingine anayestahili kuchuma matunda ya uwekezaji alioufanya kwa mwanae.

Farai kwa upande wake kipindi hicho alidai kujipanga kumuoa mama yake na atalipa sehemu ya ilobola, yaani mahari, ambayo baba yake hakuilipa kwa bibi zake.

“Najua baba yangu alifariki dunia kabla hajamaliza kulipa mahari na nimejiandaa kuimaliza ili nichukue jumla jiko langu,” alisema kwa kujiamini na kuongeza:

“Ni vyema kutangaza hadharani juu ya kinachoendelea baina yetu kwa sababu watu wanapaswa wajue kuwa ni mimi ndiye niliyemjaza mimba mama yangu. Vinginevyo wangemtuhumu ukahaba wakati si kweli.”

 

Lakini mkuu wa kijiji cha Mwenezi, Nathan Muputirwa alisema: “Hatuwezi kuruhusu uchuro huu katika kijiji chetu, hii ni dalili mbaya kwa kweli.”

Aidha, Muputirwa aliwaonya wawili hao waivunje mara moja ndoa yao au wasionekane kijijini hapo, hali iliyowafanya wakimbilie Afrika Kusini kuishi kwa raha mustarehe hadi hivi karibuni uhusiano wao umeingia shubiri.

Miaka mitano tangu uchuro ufahamike hadharani, wawili hao wametalikiana baada ya Farai kudai amegundua mama yake alitumia uchawi na kumfanya kutekeleza uchuro huo.

Lakini mama huyo hajasema chochote kuhusiana na kisa hicho.

Farai anadai kugundua hilo alipomtembelea mchungaji mmoja nchini Afrika Kusini kwa jina Pastor Mboro ambaye alimwombea na kumfungua macho yake.

Walioshuhudia kisa hicho walieleza kuwa Farai alianguka chini wakati wa maombi na kuanza kutapika, hali iliyomvuta mchungaji huyo kwake.

Alipoanza kumwombea, uchawi huo ulitoka, ambapo alifunguka macho.

Farai alisema: “Mwanamke huyu ni mbaya sana, alikuwa ameniroga kwa miaka hii yote. Na nagundua sasa kwanini alinisisitiza nile nyumbani kila siku!”

Kwa mujibu wa Farai alifikiria alikuwa anampenda mama yake lakini hakujua kuwa alikuwa anamwekea ‘juju’ ndani ya chakula ili aendelee kuwa naye.

“Wakati kuna wanawake wa umri mdogo na warembo inakuaje nimuoe mwanamke mzee kama mamangu. Nimebadilisha nambari yangu ya simu na sitaki kumwona tena,” anasema.

Wakati wanahabari walipompigia mama yake Betty kuhusu kilichotokea hakuwa tayari kuzungumza zaidi ya kumwaga mitusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles