23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Unajua sababu za mpenzi wako kutaka ubadili tabia yako?

ZAIDI ya asilimia 47 ya watu walio katika uhusiano, wanaombwa na wapenzi wao wabadilike kitabia. Japo siyo kila tabia kitaalamu unapaswa kuibadili hata kama mwenzako anakwambia japo asimilia kubwa ya tabia za wahusika zinapaswa kubadilika.

Ila swali la msingi, huwa unamuelewa mwenzako anapolalamika kwamba anataka ubadilike? Unajua anataka nini katika mabadiliko yako?

Ifahamike, mara nyingi mwenzako anapotaka ubadilike, kuna kitu ama vitu vinamkera katika tabia yako. Hivyo kilio chake cha kutaka ubadilike ni kuhitaji uachane na vitu hivyo ili afurahie zaidi kuw ana wewe katika uhusiano. Kilio cha mwenzako juu ya mabadiliko ya tabia yako mara nyingi huwa ni kwa faida yako na yake.

Mfano, labda anahisi unamsaliti kutokana na tabia yako fulani. kilio chake cha kutaka ubadilike tafsiri yake ni kwamba anataka kuwa na amani na furaha na wewe. Kama ukiachana kubadilika, hawezi kuwa na furaha na amani. Unajua tafsiri ya yeye kutokuwa na furaha akiwa na wewe?

Mwenzako akiacha kuwa na amani na wewe kwa sababu ya kutokuwa na imani juu ya tabia yako juu yake, huenda pia asione sababu na maana ya yeye kuendelea kuwa muaminifu na mwenye kukuheshimu. Athari ya jambo hili ni yeye kuwa mtu wa hovyo kwa sababu ana amini na wewe pia ni mtu wa hovyo kwake.

Kumbuka binadamu huwa anaziamini na kuheshimu zaidi hisia zake kuliko maneno anayoambiwa. Hivyo ni vema kuwa na tabia ama mwenendo unaochochea hisia chanya kwa mwenzako kuliko hasi.

 Ni kosa kubwa kuacha kufikiria kwanini mwenzako anataka ubadilike. Ni kweli, siyo kila jambo mwenzako analokwambia halitaki basi unapaswa kuliacha. Hawezi kukwambia acha kupokea simu ya bosi wako ama ya wateja wako unapokuwa nyumbani kisha na wewe ukakubali kwa kigezo cha kutaka kumfurahisha.

Ila pia ni vema kumueleweshwa mwenzako juu ya umuhimu wa kupokea simu hizo na siyo kuonyesha dharau juu yake.

 Unapoonesha dharau kwa mwenzako, unahamasisha hisia za mwenzako ziamini kwamba yeye sio wa muhimu na hana thamani kwako. Kitu hiko sio tu kitamfanya aumie ila pia kitamfanya  ajione yuko sehemu isiyo sahihi katika maisha yake.

Kilio cha mwenzako juu ya mabadiliko ya tabia yako inabidi ukipe nafasi muhimu katika akili yako. Mpaka mwenzako anakutaka ubadilike ujue tabia yako fulani inamfanya asiwe na amani na furaha. Sasa mtu ataendelea vipi kujivuia wewe katika maisha yake na humfanyi kuwa na amani na furaha?

 Mahusiano yanapaswa kuwa sehemu ya kufurahishana, kupeana hamasa ya maisha na kubadilishana raha. Kama humfanyi mwenzako kupata vitu hivyo kwa sababu ya tabia yako, abadani hawezi kujiona yuko katika mahusiano kamili.

 Na kama mtu asipojiona yuko katika mahusiano kamili unajua nini kitafuata? Binadamu toka enzi za kale ni mtu mwenye kuhangaika kutafuta sehemu ya kumpa, furaha amani na pumziko. Kama kwao pia anaona sio sehemu ya kumfanya ajidai, sio ajabu sana kuhama na kuondoka kusaka sehemu bora zaidi.

 Mahusiano mengi yanapovunjika ni kwa sababu wahusika hawapeani yale wanayotarajia kwa kila mmoja. Kama mwenzako analitarajia kupata raha na utulivu kwa kuwa na wewe na anaona hapati, unafikiri atakuwa na sababu gani ya kuendelea kuwa na wewe?

Kuwa chanzo cha raha kwa mwenzako ikiwa unahitaji aendelee kuwa sehemu ya maisha yako. Hakuna mtu anayeingia katika mahusinoa ili apate karaha na maudhi. Iangalie vema tabia yako kama inampa mwenzako sababu ya kujivunia kuwa na wewe.

Instagram: g.masenga

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia ( Psychoanalyst)

  [email protected]

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles