31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

UN yazindua mpango mpya wa kudhibiti ugaidi

Umoja wa Mataifa umezindua mpango wa kudhibiti ugaidi kwa kufuatilia wasafiri ili kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuboresha uwezo wa kubaini na kuzuia safari za magaidi.

Kupitia ofisi ya kukabiliana na ugaidi, UNOCT, uzinduzi huo umefanyika wakati wa kikao cha ngazi ya juu kilichofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema mpango huo unaohusisha kuanzishwa kwa vitengo vya safari katika nchi husika, umekuja wakati muafaka kwa kuwa zama za sasa kuna mienendo mingi inayohusisha wapiganaji wa kigeni na magaidi kusafiri kutoka kona moja hadi nyingine ya dunia.

“Miaka miwili tu iliyopita, tulikadiria kuwa zaidi ya wapiganaji magaidi wa kigeni 40,000, kutoka zaidi ya nchi 110 walisafiri kujiunga na makundi ya kigaidi nchini Syria na Iran. Na kufuatia kitendo cha magaidi wa ISIL kufurushwa kwenye maeneo yao, magaidi wengi wanajaribu kurejea nyumbani au wanasaka maeneo salama au kwingineko kwenye mapigano,”amesema Guterres.

Amesema wengi wao wana mafunzo ya hali ya juu wanaweza kufanya mashambulizi na wengine wana matumaini ya kusaka wafuasi wapya, kwa hiyo, “kuwabaini na kusambaratisha magaidi hawa na wahalifu wengine hatari kabla hawajafanya shambulio ni kipaumbele cha jamii ya kimataifa.”

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, mpango huo “utasaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kukusanya, kuchakata na kubadilishana taarifa za safari na mamlaka nyingine bobezi za kitaifana kimataifa huku wakiheshimu faragha na masuala mengine”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles