27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

UN yazindua mkakati wa vijana kuelekea 2030

Mwandishi Wetu, New York

Umoja wa Mataifa (UN), umetengeneza historia kwa vijana duniani kwa namna ya pekee kwa kuzindua mkakati wa vijana kuelekea 2030 ikiwa ni moja ya matukio yaliyosubiriwa kwa hamu kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 73 ulioanza leo hapa New York nchini Marekani.

Mkakati huo umezinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio Guteres ambapo amesema ni mkakati uliofikiriwa na Umoja huo wa kufanya kazi na vijana kwa ajili ya vijana na kuwapa kipaumbele katika mambo ya msingi katika kutimiza mpango wa maendeleo endelevu.

“Ni wazi kuwa katika dunia ya sasa kuna takribani vijana bilioni 1.8 wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 24 likiwa ni kundi kubwa la vijana kuwahi kutokea katika historia ambapo wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na mambo kama utandawazi, kukua kwa teknolojia na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Vijana wengi hawako katika ajira shuleni au hata katika mafunzo huku mmoja kati ya wanne akiathiriwa na vurugu za vita kwa namna moja ama nyingine, mamilioni ya wasichana wanapata watoto katika umri mdogo jambo linaliothiri afya zao na kuendeleza mzunguko wa kubaki katika lindi la umaskini,” amesema.

Amesema jambo la kushangaza ni kwamba vijana hao kwa kiasi kikubwa hawashirikishwi katika masuala kimaendeleo sambamba na kunyimwa sauti na viti katika ngazi za maamuzi huku wakiwa ni chanzo cha ubunifu, mawazo chanya na suluhisho katika mambo mengi wakipatiwa nafasi.

Mkakati huo wa vijana umelenga mambo makuu matano ya msingi katika utekelezaji wake moja ikiwa ni kufungua milango mipya katika kuwashirikisha vijana yakiwamo kuimarisha mpango wa kuhakikisha wanafikiwa na elimu na huduma bora za afya, kuhakikisha wanawezeshwa kiuchumi kupitia mafunzo na utoaji wa ajira, kuhakikisha haki zao zinapewa kipaumbele kuwashirikisha katika mambo ya kijamii na kisiasa na tano kutoa kipaumbele kwa vijana na utatuzi wa migogoro na haki za binadamu kwa kuwashirikisha katika hatua za kulinda amani.

Hata hivyo, Katibu Mkuu ametoa wito kwa nchi wanachama wa UN kuupa kipaumbele utekelezaji wa mkakati huo ili kuwaimarisha vijana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles