28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

UN yaipongeza Tanzania kwa ulinzi Maziwa Makuu

Mwandishi Wetu-New York, Marekani

NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Amina Mohammed, ameisihi Tanzania kuendelea kuimarisha amani katika Ukanda wa Maziwa Makuu na kuendelea kuchangia kutoa askari wa vikosi vya ulinzi wa amani duniani.

Dk. Amina alitoa wito huo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, New York nchini Marekani.

Alisema UN inatambua mchango wa Tanzania katika ulinzi wa amani duniani na kwamba iko tayari kushirikiana nayo kuendeleza jitihada hizo ili kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

“Tanzania imekuwa muhimili muhimu katika kuhimiza amani katika ukanda wa Maziwa Makuu, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi wakimbizi kutoka ukanda huo kwa miaka mingi bila kuchoka,” alisema Dk. Amina.

Kwa upande wake, Profesa Kabudi alisema Tanzania inatambua nafasi ya UN na itasalia kuwa mwanachama wa umoja huo.

“Napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa askari wake katika vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani,” alisema Profesa Kabudi.

Alimweleza hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepiga katika masuala ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni pamoja na afya, maji, ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi pamoja na masuala ya kuimarika kwa demokrasia.

Profesa Kabudi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani alipokuwa akimwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles