30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UN yahofia baa la njaa Afrika kutokana corona

 NEW YORK, MAREKANI

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ametahadharisha juu ya mamilioni ya watu kukumbwa na baa la njaa barani Afrika litakalosababishwa na janga la sasa la virusi vya corona.

Guterres alisema jana kuwa, kusambaa virusi vya corona barani Afrika kutaifanya jamii kubwa ya bara hilo kukumbwa na umasikini mkubwa na baa la njaa.

Sambamba na kuitaka jamii ya kimataifa kuwa pamoja na bara la Afrika Guterres alisema kuwa, tangu kale bara hilo lilikuwa likikabiliwa na dhulma, ukosefu wa uadilifu, umasikini, magonjwa mbalimbali na ubaguzi na hivi sasa kuenea virusi vya corona huenda kukawafanya mamilioni ya watu barani humo kuwa masikini zaidi na kukumbwa na na baa la njaa.

Guterres kwa mara nyingine tena aliyataka mataifa mbalimbali ulimwenguni yatekeleze ahadi zao za kutoa msaada wa kiwango cha Dola bilioni 200 kwa ajili ya kuzuia kutokea maafa ya kibinadamu barani Afrika.

Wakati huo huo, Guterres amewapongeza wote walio mstari wa mbele kupambana na janga la Covid-19 kuanzia wauguzi na wakunga, hadi wafanyakazi wa maabara, wasimamizi na mamilioni ya wahudumu wa afya kote duniani ambao amesema wanaweka rehani maisha yao ili kuokoa maisha ya wengine.

Ingawa hadi sasa ni watu 2,500 tu wameaga dunia barani Afrika kwa virusi vya corona, lakini wataalamu wa masuala ya tiba wana wasiwasi kwamba, virusi hivyo huenda vikaenea kwa kasi barani humo katika majuma yajayo na kulifanya bara hilo kukabiliwa na maafa makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles