UN waongeza muda wa uchunguzi

0
861

BUJUMBURA, BURUNDI

Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu limetangaza kuongeza muda wa mwaka mmoja kwa Tume ya Uchunguzi ya Umoja huo nchini Burundi, wakati serikali ya nchini hiyo ilikuwa imetishia kujitoa kwenye taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa kwa vyombo vya habari, imesema azimio hilo, lililopendekezwa na Umoja wa Ulaya, lilipitishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa mataifa kwa kura 23 kkati ya wajumbe kutoka nchi 47 wanachama wa Baraza hilo.

Hata hivyo wakati wa upigaji kura, nchi saba zilipinga azimio hilo na nchi 17 zilijizuia kupiga kura juu ya hatima ya Tume inayofanya uchunguzi huko Burundi.

Katika ripoti iliyochapishwa Septemba 5 mwaka huu, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu umeendelea bila hofu yoyote mwaka 2017 na 2018, vitendo ambayo vinatekelezwa hasa na idara ya Upelelezi (SNR), polisi na jeshi bila kusahau kundi la vijana kutoka chama tawala CNDD-FDD, Imbonerakure.

Azimio hilo limelaani vitendo vyote vya vurugu vinavyoendelea kutekelezwa nchini Burundi na pande zote, au na watu na kuamua kuongeza muda wa mwaka mmoja kwa Tume hiyo ili iweze kuendelea na kuchunguza kwa kina.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi, Doudou Diene, katika taarifa yake juu uamuzi wa Baraza la Haki za Binadamu amesema ni jambo lenye heri na amelikaribisha kwa mikono mwili.

Tume hii iliundwa mnamo mwaka 2016 na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, lakini serikali ya Burundi kamwe kuijairuhusu kuingia nchini humo, hadi kutishia maafisa wa uchunguzi kwamba itawafungulia mashitaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here