Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema vyombo huru vya habari ni muhimu kwa amani, haki, maendeleo endelevu na haki za binadamu.
Maudhui ya mwaka huu ni “Vyombo vya Habari kwa Demokrasia: Tasnia ya Habari na Uchaguzi katika Nyakati za Upotoshwaji wa Taarifa.”
Guterres amesema, “hakuna demokrasia iliyo kamilifu bila kupata taarifa kwa uwazi na za kuaminika. Ni msingi wa kujenga taasisi za haki za zisizo na upendeleo, na kuwawajibisha viongozi na kila wakati kueleza mamlaka ukweli.”
Ameongeza kuwa taarifa za uwazi na za kuaminika ni ni muhimu zaidi wakati wa msimu wa uchaguzi, ambayo ndio maudhui ya sik uya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani mwaka hu una kwamba , “taarifa sahihi na si za uongo zinapaswa kuongoza watu wakati wanachagua wawakilishi wao.”
Hata hivyo amesema wakati teknolojia imebadili jinsi tunapokea na kubadilishana taarifa, wakati mwingine inatumika kudanganya maoni ya umma au hata kuchochea ghasia na chuki.