25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Umoja wa Mataifa: Corona ni mtihani mkubwa tangu WWII

 NEW YORK, MAREKANI

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) António Guterres ameonya kuwa mlipuko wa sasa wa virusi vya corona (Covid 19) ndiyo changamoto kubwa kwa ulimwengu tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia (WWII).

Amesema mlipuko huo unaweza kuleta kushuka kwa uchumi “ambayo labda hauwezi kufananishwa katika siku za nyuma za hivi karibuni”.

Akiongea katika makao makuu ya UN huko New York wakati wa uzinduzi wa ripoti juu ya athari kubwa ya kiuchumi ya mlipuko huo, Guterres alisema ugonjwa huo mpya wa corona unashambulia jamii kwa kwa kishindo, kusabbisha vifo vya watu na kuathiri maisha yao.

Alisema nchi zote ulimwenguni zimeweka safu za uchukuaji hatua, ikiwa ni pamoja na kuzuia atu kutembes na kukusanyika na kufunga biashara nyingi, ili kupunguza kuenea kwa virusi hivyo.

Ripoti ya UN inakadiria kwamba hadi kazi milioni 25 zinaweza kupotea ulimwenguni kote kama matokeo ya kuzuka. Pia miradi inayokadiriwa kufikia asilimia 40 inayofadhiliwa katika nchi mbalimbali kwa ajili yakuchochea uchumi inatarajiwa kuporomoja.

“Covid-19 ni mtihani mkubwa kabisa ambao tumekabili pamoja tangu kuumbwa kwa Umoja wa Mataifa. Tunahitaji mwitikio wa afya ulioratibiwa mara moja ili kukomesha maambukizi na kumaliza janga,” alisema.

Onyo lake linakuja wakati wa utabiri mkali juu ya uwezekano wa athari za kiuchumi za hatua zilizowekwa kupambana na virusi hivyo.Idadi ya kesi zilizothibitishwa ulimwenguni kote sasa inakaribia 860,000, na zaidi ya vifo 42,000.

Idadi ya vifo nchini Marekani tayari sasa ni zaidi ya 4,000 zaidi ya idadi ya waliouawa nchini China, ambapo ugonja huo ulianzia mwishoni mwa mwaka jana.

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimesema watu 865 walikuwa wamefariki dunia katika masaa 24 yaliyopita nchini Marekani na kwa watu wote zaidi ya 189,000 nchini humo wameambukizwa.

Wakati huo huo, Hispania inaikaribia Italia kwa idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya kushuhudia vifo 849 katika masaa 24 kufikia jana, idadi kubwa zaidi ambayo imekuwa nayo katika siku moja.

Nchini Uingereza, jumla ya watu 1,789 wamefariki dunia, ikiwa ni ongezeko la watu 381, maofisa wanasema. Kati ya waathiriwa ni kijana wa miaka 13, kwa mujibu wa Hospitali ya Trust King’s College ya mjini London.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles