UMMY MWALIMU AMSIMAMISHA KAZI MGANGA MKUU MLANDIZI

0
1110

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, amemsimamisha kazi Mganga Mkuu Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi, Stanley Tamambele ya kwa kushindwa kuwasimamia wauguzi na madaktari wa kituo hicho.

Tamambele amesimamishwa leo Julai 25, baada ya kubainika wauguzi na madaktari wa kituo hicho wamemtoza fedha kiasi cha Sh,180,000 mjamzito Salma Halfan kwa ajili ya kununulia vifaa ya upasuaji wakati vifaa hivyo vinapatikana kituoni hapo.

Mwalimu, ambaye alikuwa katika  ziara yake ya kukabidhi magari matatu ya wagonjwa yakiwemo magari mawili yaliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa (CCM) na Rais John Magufuli aliyetoa gari moja na vitanda vitano vya kujifungulia.

Awali, kabla ya Mwalimu kukabidhi magari hayo alitembelea kituo hicho ambapo alikutana na Salma ambaye alikuwa amejifungua kwa upasuaji huku akidai ametozwa kiasi hicho cha  fedha hali iliyomshangaza waziri na hivyo kutaka daktari na muuguzi aliyetoza fedha hizo kurudisha haraka.

Katika mazungumzo yake na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini Mwalimu alisema kuwa Serikali imewasamehe wajawazito na hivyo wanapaswa kutibiwa bure bila kulipa fedha yoyote hivyo jambo walilofanya kituoni hapo nilakushangaza na kwamba lazima wahusika wachukuliwe hatua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here