23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Ummy ataka wenye fistula wajitokeza kutibiwa bure

Na Mwandishi wetu

-Dodoma

WANAWAKE wenye fistula nchini wametakiwa kuacha kujifungia ndani na badala yake waenda kupata matibabu katika hospitali zilizoainishwa na Serikali.

Hayo yamesemwa jana Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya fistula duniani inayoadhimishwa Mei 23.

Alisema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2018 zinaonyesha wanawake millioni mbili  wanaoishi na fistula duniani kote.

Inakadiriwa wagonjwa wapya kati ya 50,000 na 100,000 hupatikana kila mwaka, wakati juhudi za kutibu fistula ulimwenguni kote huishia kutibu wagonjwa 20,000 tu. 

Kwa upande wa Tanzania, Ummy alisema inakadiriwa wanawake 2,500 wanapata fistula kila mwaka, huku idadi ya wanaopatiwa matibabu ikiwa ni  1,000.

“Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi Disemba, 2019 wanawake zaidi ya 5,500 wametibiwa Fistula. Mafanikio haya yanatokana na kampeni iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Serikali na wadau ambayo imeweka mabalozi wa fistula zaidi ya 3,000 nchi nzima wanaosaidia kuratibu rufaa na usafiri kwa wagonjwa kwenda hospitali zinazotoa huduma ya fistula,”alisema Ummy.

Ummy aliwataka akinamama wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu anapojihisi mjamzito ili kuweza kuchunguza afya yake pamoja na mtoto.

“Mama mjamzito endapo atawahi kliniki mapema kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake na mtoto na kuhakikisha anajifungulia katika kituo cha kutolea huduma za afya atapunguza uwezekano wa kupata tatizo la fistula. 

“Nitumie fursa hii kuendelea kuhimiza akina mama wajawazito kuwahi kliniki mapema, kukamilisha mahudhurio yote manne na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya,”alisema i Ummy.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles