29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Ummy ahaidi kuchochea ujenzi wa viwanda Tanga

Na OSCAR ASSENGA-TANGA

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema endapo akichaguliwa atachochea ujenzi wa viwanda vipya katika Jiji la Tanga ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana na akina mama ili kukuza uchumi.

Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyanjani Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni.

Alisema kwamba hilo litafanikiwa kutokana na kuwa na mtandao wa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hivyo ataweka msukumo wao kuja Jijini Tanga kujenga viwanda ili akina mama waweze kupata ajira na vijana.

Mgombea huyo alisema viwanda vikipatikana vitachangia fursa za ajira kwa watu wa kada zote.

“Lakini jambo la pili ni nitainua uchumi wa Tanga na kusukuma uboreshaji wa Bandari ya Tanga” alisema Ummy huku akimshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kuupatia mkoa huo Sh bililioni 372 ili kuboresha Bandari ya Tanga.

“Hivyo niwaombe wana Mnyanjani mnichague ili nikasukume maboresho ya awamu ya pili ya Bandari ya Tanga tuweze kuona meli kubwa zikitia nanga kwenye Bandari ya Tanga,”alisema.

 Alisema meli zikitia nanga kwenye Bandari hiyo itasaidia kufungua fursa za ajira kwa wananchi na hivyo kuinua uchumi wa wakazi wa Jiji la Tanga .

“Lakini Bandari ya Tanga ikiboreshwa nitapigania mizigo yote inayoingia nchini na kwenda mikoa ya Kanda ya Kaskazini ishushwe kwenye Bandari ya Tanga badala ya Dar es Salaam,”alisema

Alisema  ameamua kugombea ubunge ili aweze kuwatumikia wana Tanga sambamba na kuchochea mradi mkubwa wa ujenzi wa bombo la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles