Umasikini chanzo cha watoto kutosoma

0
845

mimba

ALLY  BADI,  KILWA

UMASIKINI wa kipato,kilimo cha kuhamahama  kwa  baadhi ya wazazi na walezi kudaiwa kunachangia watoto wasiandikishwe shule  na  uwapo wa maendeleo duni ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Hayo  yamesemwa wakati wa  utafiti  uliofanywa  na  Shirika la Action Aid na kuwasilishwa  mtafiti, Jacob Kateri  katika kikao kazi na wadau wa elimu kilichofanyika  Kilwa  masoko,chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai.

Akiwasilisha ripoti hiyo juzi, Kateri alisema utafiti uliofanywa kati ya shirika hilo na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali la Wilaya ya Kilwa (KINGONET),umebaini uwapo wa changamoto mbalimbali zikiwemo za umasikini wa kipato.

Alisema kitendo cha wazazi na walezi kutotambua na kuthamnini umuhimu wa elimu,kunachangia washindwe kuchangia kuinua kiwango cha elimu, ikiwemo  pamoja na kujitokeza kushiriki,kujenga nyumba za kuishi walimu,vyumba vya madarasa na vyoo.

Alisema umasikini wa kipato kwa baadhi ya wazazi na walezi kunachangia wanafunzi wanaosoma shule mbalimbali, zikiwamo za msingi na sekondari washindwe kuwapatia vijana wao mahitaji muhimu kama vile chakula na gharama zingine.

Alisema sababu nyingine  kuendelea kwa adhabu ya viboko  kwa wanafunzi ni changamoto  zilizopo  katika shule z wilaya  humo, kwani kati ya Shule (15) zilizokuwa zimefanyiwa utafiti (14) zimeelezewa  ni suala la kawaida,shule tatu zimetaja uwapo  ukatili wa kingono na ukatili wa kimwili.

Alisema   upungufu wa walimu na wengine kuishi mbali na maeneo yao ya kazi,nalo ni tatizo walilobaini na kuomba uongozi husika kulifanyia kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here