31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ULAYA YATOA TAMKO ZITO WATU KUPIGWA RISASI, KUUAWA

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UMOJA wa Ulaya (EU) kupitia ofisi zake umetoa tamko kukemea matukio yenye viashiria vya ukatili na vitisho hapa nchini.

Tamko la EU limetolewa baada ya hivi karibuni Ubalozi wa Marekani hapa nchini kutaka kufanyika uchunguzi ulio wazi wa tuhuma za kuuawa kwa Katibu wa Chadema, Kata ya Hananasif, Daniel John.

Taarifa iliyotolewa na EU kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana kwa ushirikiano na mabalozi wa nchi wanachama wenye uwakilishi hapa nchini na kuungwa mkono na mabalozi wa nchi za Norway, Canada na Uswisi.

“Tunashuhudia kwa wasiwasi muendelezo wa matukio ya hivi karibuni yanayotishia nidhamu ya demokrasia na haki za Watanzania, katika nchi iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa utulivu, amani na uhuru.

“Tumesikitishwa na kifo cha mwanafunzi aliyepigwa risasi mwisho wa juma lililopita, Akwilina Akwilini, anayeombolezwa nchi nzima, tunakaribisha wito wa Rais Dk. John Magufuli wa uchunguzi wa haraka,” ilieleza.

Pia taarifa hiyo ilitoa wito wa uchunguzi wa kina katika vifo vyote vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu na tunatoa pole za dhati kwa familia zao zote.

“Tuna wasiwasi na ongezeko la ripoti za ukatili katika miezi ya hivi karibuni, kama vile, jaribio lililohatarisha maisha ya Mbunge Tundu Lissu; kupotea kwa watu kama mwandishi wa habari Azory  Gwanda pamoja na mashambulio yaliyopoteza uhai wa viongozi wa Serikali, wawakilishi wa vyombo vya usalama na wananchi yaliyotokea Pwani ndani ya miaka miwili iliyopita,,” ilieza taarifa hiyo.

Pia alisema wanaungana na Watanzania kuwaomba wahusika wote, kutunza amani na usalama wa michakato ya kidemokrasia, nchi, watu wake na kuheshimu utawala wa sheria bila udhalimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles