ULAYA, CHINA KULINDA MKATABA WA PARIS

0
666

 

 

BRUSSELS, UBELGIJI

UMOJA wa Ulaya (EU) na China umeahidi tena kuendeleza Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Paris 2015, siku moja baada ya Marekani kutangaza kujitoa katika makubaliano hayo.

Katika mkutano wa pamoja, EU na China zimesema mabadiliko ya hali ya hewa na nishati safi itakuwa ni nguzo yao muhimu katika ushirikiano wao.

Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, amesema juhudi za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa zitaendelea, bila ya kujali kuwepo au kutokuwepo kwa Marekani.

“Leo China na EU zimeonyesha mshikamano wao kwa kushirikiana na kizazi kijacho na majukumu ya kusimamia dunia yote. Tunaamini kuwa uamuzi uliofanywa jana ni kosa kubwa,” alisema Tusk.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang, akiwa Brussels kwa ajili ya mkutano wa kibiashara kati ya EU na China, amesema ni jambo muhimu kwa mahusiano ya China na EU kuimarishwa zaidi.

“Tunaamini kuwa kumekuwa na mabadiliko katika medani za kimataifa na kutaendelea kuwepo mashaka na sababu za kutuyumbisha,” alisema.

 “Hili linatutaka tuongeze juhudi zetu ili kutatua mambo haya yanayotukabili.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here