29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

ULAJI NYAMA YA NYANI WATISHIA UTALII

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

VITENDO vya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa iliyopo Morogoro hususani uwindaji wa nyani wa kitoweo, unaweza kupunguza mapato yatokanayo na  shughuli za utalii.  

Kwa miaka mingi watalii na baadhi ya watafiti wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kufanya utafiti na kujionea makundi 11 ya nyani wa aina mbalimbali wakiwamo pekee aina ya Sanje Mangebay na Iringa Colabus wanaopatikana hifadhini humo.

Hayo yalisemwa juzi na Muikolojia Msaidizi wa Hifadhi ya Udzungwa, Christine Kibwe alipokuwa akizungumza kupitia makala za utalii zinazoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kurushwa na Kituo cha televisheni ya Taifa (TBC) juzi.

Alisema wanaendelea kukabiliana na changamoto ya kuwahifadhi nyani hao adimu kutokana na baadhi ya watu wanaowatumia kama kitoweo.

“Nyani hawa wa kipekee kabisa wanastahili kutunzwa na kulindwa vizuri kwa ajili ya kuliingizia taifa kipato zaidi,” alisema Kibwe na kuongeza:

“Jamii inayotuzunguka imekuwa ikiwatumia nyani kama kitoweo kwa hali hiyo kama hatutaweza kufuatilia kwa karibu basi wanaweza kusababisha kutoweka kwao,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Hifadhi hiyo, Hassan Nguluma alisema kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipokea watalii kutoka nje badala ya wananchi waishio nchini.

“Watanzania hawana mwamko wa kutembelea na kujionea rasilimali walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu, kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukipokea watalii kutoka nje ya nchi badala ya watalii wa ndani wazawa,” alisema.

Nguluma alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna aina mbili za nyani ambao hawapatikani sehemu nyingine duniani ambao ni Sanje Mangebay na Iringa Colabus.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles