22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

UKUTA WA TANZANITE WAINGIZA MILIONI 700

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, serikali imepata mapato ya Sh milioni 714  ikilinganishwa na Sh milioni 147.1 zilizopatikana kwa mwaka wote wa mwaka 2017.

Amesema hali hiyo inatokana na hatua zilizochukuliwa baada ya kuimarisha ulinzi wakati wa ujenzi wa ukuta kwenye migodi ya Tanzanite, huko Mirerani mkoani Manyara.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi yake, kwa mwaka 2018/19, Majaliwa amesema; “mapato hayo yameongezeka tu baada ya kuimarisha ulinzi wakati wa ujenzi wa huo ukuta.”

Amesema mbali na manufaa hayo, pia katika eneo hilo la Mirerani zitajengwa nyumba za kuuzia madini hayo jambo litakalokuwa na manufaa kwa wananchi wa eneo hilo pia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles