29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Ukuta wa Mirerani uliojengwa na JPM waongeza makusanyo

Na Mwandishi Wetu, Manyara

Ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite uliopo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara, uliojengwa na Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli, umesababisha kuongeza makusanyo na kukomesha wizi na utoroshaji wa madini hayo.

Ofisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Mirerani, Fabian Mshai ameyasema hayo Mji mdogo wa Mirerani kwenye sala na dua ya kumuombea hayati Magufuli kwenye maombolezo yaliyofanyika kwenye lango la ukuta unaozunguka migodi hiyo.

Ofisa madini Mkazi Mkoa wa kimadini wa Mirerani, Fabian Mshai akizungumza kwenye sala na dua ya kumuombea apumzike kwa amani Rais wa awamu ya tano hayati Dokta John Magufuli, kwenye maombolezo yaliyofanyika nje ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Mshai amesema awali kabla ya ukuta huo kujengwa mapato ya madini ya Tanzanite yalikuwa chini kwani walikuwa wanakusanya Sh milioni 238 kwa miaka miwili ya 2016 na 2017.

Amesema baada ya kujengwa ukuta huo na kukamilika mwaka 2018 mapato yakiongezeka na kufikia Sh bilioni 1.4 na mwaka 2019 ikafikia Sh bilioni 2.1.

Amesema hayati Magufuli atakumbukwa kwa mambo mengi ya maendeleo kwenye sekta ya madini ndiyo sababu wameungana na wadau wa madini kufanya sala na dua pembeni ya ukuta huo ili kumuombea apumzike kwa amani.

Ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite wenye urefu wa kilomita 24 ulianza kujengwa mwaka 2017 na kukamilika mwaka 2018 na kugharimu Sh bilioni 5.

Ukuta huo uliojengwa kwa muda wa miezi mitatu na askari wa JKT ulikamilika na kufunguliwa baada ya miezi sita ya tamko la hayati Magufuli.

Diwani wa Kata ya Mirerani, Salome Mnyawi amesema hayati Dk. Magufuli alipojenga ukuta huo amesababisha wanawake wadau wa madini kufanya kazi zao kwa usalama tofauti na awali.

Katibu wa chama cha wachimbaji madini Mkoani Manyara MAREMA Tawi la Mirerani, Rachel Njau amesema hayati Dk. Magufuli ndiye amesababisha mchimbaji mdogo akatambulika kuwa naye ni mdau wa maendeleo kupitia sekta binafsi.

Diwani wa kata ya Endiamtu, Lucas Zacharia amesema hayati Dk. Magufuli ndiye amesababisha yeye akaingia kwenye siasa kipindi akiwa Waziri wa uvuvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles