23.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

‘UKUSANYAJI KODI ZA MAJENGO IRUDISHWE SERIKALI ZA MITAA’

Elizabeth Hombo, Dodoma


Kamati ya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango, imeishauri serikali kurudisha jukumu la ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa serikali za mitaa.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni amesema wanatoa ushauri huo kwa sababu bado Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) haijawa na uwezo wa kutosha kukusanya chanzo hicho.

Makamu Mwenyekiti huyo amesema hayo le wakatia akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango.

“Kamati inaishauri serikali kurudisha chanzo hiki katika mamlaka ya serikali za mitaa kwa sababu bado mamlaka ya mapato haijawa na uwezo wa kutosha kukusanya chanzo hiki.

“Pili ni utaratibu wa kutumia dhamana ya serikali za mitaa katika kupata fedha za maendeleo kwa serikali za mitaa utashindikana kwa sababu halmashauri hazitakuwa na uwezo wa kulipa riba pindi amana hizo zinapoiva.

“Tatu kamati inaishauri serikali kutumia wanafunzi wa Chuo cha Ardhi kufanya shughuli ya kufanya tathimini ya majengo wakati wa mafunzi ya vitendo ili kuongeza tija ya ukusanyaji wa mapato husika,” amesema.

Aidha amesema tathimini ya ujumla ya mwenendo wa utaoaji wa fedha za utekelezaji bajeti ya mwaka 2017/18 si wa kuridhisha kwa baadhi ya mafungu.

“Hadi kufikia Machi mwaka huu kati ya mafungu nane yaliyo chini ya Wizara ya Fedha, ni mafungu mawili tu yalikuwa yamepokea fedha zaidi ya asilimia 60 ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles