30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

UKUBWA SI UMRI, KAMA HUNA HEKIMA TUNAKUZINGUA TU

Na RAMADHANI MASENGA

WANANGU, ukiona mtoto mdogo anamtukana mtu mzima ujue huyo mtoto hana adabu wala madili, ila  ukiona mtu mzima anamrudishia matusi mtoto mdogo ujue mtu mzima huyo hamna kitu kichwani.

Utu mzima si ukubwa wa namba wala idadi ya mvi kichwani. Ukubwa ni hekima na maamuzi ya msingi. Kama mtu mzima, unaamua kijinga kama mtoto mdogo basi utaheshimiwa kwa ukubwa wa namba za umri wako ila una haki ya kudharauliwa kutokana na uchache wa hekima yako.

Masela naongea haya kutokana na vitimbi vingi vinavyotokea kitaa. Umeona wapi maza ama faza makini akachekelea ama kutetea upimbi wa mwanaye, hata awe anampenda vipi?

Mzazi mwenye kutetea uzumbukuku wa mwanaye siyo tu kuwa si ishara ya mapenzi  ila pia ni ishara ya udumavu wa akili yake na uchache wa tafakuri.

Mzazi mwenye kutetea ujinga wa mtoto wake ni sawa na yule anayekataa mwanaye asichomwe sindano hospitali hata kama hiyo ndiyo njia peke ya matibabu, kwa kuhofia mwanaye asipatwe na maumivu.

Kuogopa maumivu ya kidole leo, ni chanzo cha kukumbana na maumivu ya mkono mzima kesho. Kwa namna yoyote, kama mzazi zina chaji kichwani ni lazima awe mkali na shupavu kama askari kwa tabia ya mwanaye.

Mzazi magumashi ni yule anayemchekea mwanaye kwa lolote hata kama analofanya ni hatari kwake na jamii kwa ujumla. Wanangu mnanisoma kwanza? Ok.

Kuna baadhi najua mtakuwa mmepigwa na butwaa mkidhani nimepotea njia. Wanangu ni mimi yule yule kamanda wenu wa siku zote, kamanda konki, kamanda mwenye madini adimu kama Dokta Kusimano.

Nimeamua kuwasanukia kwa mtindo huu kwa ajili ya kina Bi mkubwa fulani wanaozogoa kitaa. Eti unakuta bi mkubwa anamlea mwanaye kiboya kwa kudhani anampenda bila kujua anamwingiza chaka.

Mzazi timamu ni yule ambaye hacheki na mtoto wake anapofanya ujinga. Ila mzazi magumashi ni yule anayepigana na jirani yake aliyekuwa akimuadhibu mwanaye kutokana na tabia fulani ya kijinga.

Ukiona mzazi anamchukia mtu mwenye nia ya kumrekebisha binti ama mtoto wake wa kiume, ujue mzazi huyo ni janga.

Tatizo kuwa mzazi sio suala linalohitaji cheti wala kipimo fulani kinachohusisha akili. Na kutokana na kitu hiki, ndiyo maana hata wagonjwa wa akili mtaani unakuta wanalea matumbo baada ya masela fulani kufanya yao.

Mazazi makini hawezi kuhama nyumba eti kisa mwanaye kaadhibiwa na wapangaji wenzake ama na mwenye nyumba kisa ujinga fulani aliofanya. Ila mzazi makini ni yule anayemkanya  mwanaye na kumuonya kwa ukali juu ya tabia fulani ya kijinga anayoifanya.

Ikumbukwe ukijiangalia kwenye kioo na kuona sura yako haijapendeza tiba yake sio kuvunja kioo, tiba ni kujipamba upya kisha utang’aa na kupendeza.

Mtu mkini ni yule anayekubali anapokosea na kujirekebisha ila mtu mjinga ni yule mwenye kutafuta visingizo kwa kila analokosea. Next time wana kama vipi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles