28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

UKO WAPI UTITIRI WA NGOMA ZETU?

musoma

MAISHA hayarudi nyuma, yakipita yamepita, lakini historisa ndiyo inayoweza kuturudisha nyuma tupendavyo.

Ndiyo na sisi tumnavyorudishwa miaka ya nyuma kupitia ukurasa wetu mashuhuri wa Kijaruba, ambao kwa hakiia sasa umeanza kujukuu.

Umejukuu kutokana na ukongwe wake, ulioufanya upite zile zama za watoto, sasa tunazungumzia vijukuu.

Leo tunakumbuka hasara kubwa tuliyonayo mbele yetu, ni ile iliyotufanya tupoteze baadhi ya mambo yetu adhimu yaliyokuwa yakitimiza utaifa wetu.

Yani utamaduni, au kwa neno jepesi ni kule kusahaulika kwa ngoma zetu za asili zilizokuwa zikitutambulisha katika mataifa mengine.

Watanzania tulikuwa mstari wa mbele, tukijinasibu kwa mataifa ya wenzetu kutokana na utajiri mkubwa wa ngoma zetu za makabila.

Achilia mbali maonyesho yaliyosikizwa na magwiji wa kupiga ngoma kama vile Hayati Moris Nyunyusa, wachezea nyoka akina Juma Songoroka, waimbaji taarab asilia akina Bi Kidude, hayati Shakila said na wengine lukuki.

Kwa vijana wa Kitanzania nao waliendelea kurithi mikoba ya wakongwe wakakdumisha ngoma za asili hadi kwenye miaka ya kati kati ya 80.

Tanzania ikaibuka na makundi makubwa ya muziki wa asili kama vile kundi la Tatu Nane, kadhalika vikundi vya ngoma kama DDC Kibisa, Makutano Dancing Troup, Super Fanaka, Reli Kiboko yao, Muungani Culture, JWTZ, Bima Taarab na vingine vikachipua kama uyoga.

Tukawashuhudia Manju wapya wa muziki wa asili akina Nobert Chenga, Ali Chitanda, Mzee Bakari Mbelemba au Jangala na wengine wakikusanya mashabiki wa Kitanzania katika maonyesho ya makundi mbalimbali waliyoyaunda.

Hususan jiji la Dar lilikuwa liokiwaka moto kila siku za Jumamosi kutokana na kelele za ngoma kusikika kila mtaa, huku wakazi wake wakipata burudani na elimu juu ya ngoma zao.

Haikuwa tabu tena mtoto wa kabila la Kirugulu kumuuliza baba yake asili gani ya ngoma yao, maana magwiji hao walikuwa wakizipiga na hata kueleza Jiografia ya kule zilikotokea.

Burudani na elimu hii ikaendelea kuwasaidia sana hata wasanii wenyewe kwani mialiko ya nje ya nchi ilizidi kuongezeka, lakini hata maonyesho ya ndani ya nchi nayo yalitunisha mifuko yao kwa kipato kwani mashabiki waliongezeka siku hata siku.

Bahati mbaya, safari ile, burudani ile na elimu ile vimekufa kifo cha mende, miguu juu.

Hatusikii tena wala kuona ukumbi unaowaita mashabiki wakashuhudie ngoma za lizombe na kuona utundu wa mazingaombwe ya Mtanzania kama ilivyokuwa kwa akina Profesa Singila Christopher, Prf. Manoti Pesa na wengine.

Hazionekani tena ngoma za Ngongoti kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, ilihali taifa limerejea tena kwenye umasikini wa utamaduni.

Nafasi hiyo iliyoachwa imewapenyeza wenzetu wa matifa ya magharibi kwa kasi kubwa na sasa wamejizatiti katika kutangaza utaduni wao.

Ndiyo maana sasa tunashuhudia vijana wakicheza nusu utupu, wakiimba kwa staili ya kubana pua, na sauti za kuiga zisizotoa mwangwi kama walivyokuwa wakiimba Waruguru katika ngoma ya Kiamba Mbeta. Tunasubiri majaliwa ya Mungu kurudisha vibwaya nyetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles