27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ukisomea uhandisi jiandae kuwa bilionea

JOSEPH  LINO

WANAFUNZI wa elimu ya juu wanaosomea taaluma ya uhandisi au biashara wana nafasi kubwa kuwa mabilionea zaidi ya wale wanaosomea taaluma nyingine.

Aidha, wanafunzi ambao tayari wameingia katika soko la ajira katika kazi ya mauzo au biashara ya hisa ni miongoni mwa wenye fursa kubwa ya kuwa sehemu ya watu matajiri duniani.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Ajira la Aaron Wallis, ambalo utafiti wake umeangalia watu matajiri duniani zaidi ya 100 ili kuona kama kuna uwiano au uhusiano wowote kati ya taaluma yao ya kwanza na jinsi walivyokuwa matajiri au kutengeneza utajiri.

Ripoti hiyo ilibaini  kwamba kazi yao ya kwanza, kati ya mabilionea wakubwa wa juu waliajiriwa kwa mara ya kwanza katika mashirika ambayo si yao. Pia  kuna wajasiriamali ambao walianza kampuni zao wenyewe na wengine waliajiriwa katika biashara za kifamilia  vitengo vya masoko na mauzo.

Mabilionea 10 wa mwanzo kati ya 53 waliajiriwa  katika mashirika ambayo si yao, wakati mabilionea tisa tu walianza kazi yao kama mfanyabiashara wa hisa au mauzo.

Utafiti huo pia uligundua kuwa matajiri wakubwa duniani 75 kati ya watu 100 akiwemo Bill Gates, Warren Buffet, George Soros na Jeff Bezos wana elimu ya ngazi ya shahada tu.

Kati ya hao 75,  matajiri 22 walisomea shahada katika taaluma ya uhandisi akiwamo mwanzilishi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos na  mwanzilishi wa Google Larry Page. Matajiri 16 walisomea masuala ya biashara ambapo 11 wamesoma taaluma ya fedha na uchumi.

Mabilionea 30 kati ya 100 wanautajiri wa kurithi au wanafanya kazi katika biashara ya kifamilia, wakati 17 walianza kampuni zao wenyewe.

Julai mwaka huu, muda mfupi tajiri Jeff Bezos alichukua nafasi ya Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi duniani baada ya kuongezeka kwa hisa katika mauzo ya mtandao kabla ya ripoti yake ya mapato, lakini hisa zilishuka ghafla na Gates alirejea katika nafasi ya kwanza.

Bill Gates ambaye ana utajiri wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 87, amekuwa mtu tajiri  zaidi duniani tangu mwaka 2013.

Billionea huyu mwenye moyo wa kusiadia ametoa Dola za Marekani bilioni 31.1 ya utajiri wake katika kusaidia jamii kupitia taasisi mbalimbali, wakati Jeff Bezos ametoa Dola za Marekani milioni 100; hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes la nchini Marekani.

Hata hivyo, ripoti imebaini kuwa matajiri wengi katika 100 wamesomea shahada ya kwanza ya uhandisi kama orodha ilivyoeleza.

Matajiri wakubwa 22 duniani wanataaluma ya uhandisi, ambapo matajiri 16 wamesomea masuala ya biashara katika fedha na uchumi; 11 sheria; sita sayansi ya kompyuta; wanne historia; watatu falsafa; wakati siasa, lugha ya Kiingereza, Historia na Hisabati wawili huku katika masuala ya dawa akiwa mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles