22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Ukiona mpenzi wako yupo hivi mwepuko ni laghai – 2

relationship_trouble_withholdBINADAMU tunapenda kupendwa, na tukipenda tunajisahau hivyo tunashindwa kuchunguza kama hawa tulio nao ni sahihi au la.

Wiki iliyopita tulizungumzia mambo mbalimbali ambayo yanaweza kukupa ishara kuwa huyo uliyenaye hana mapenzi ya kweli, ni laghai.

Wiki hii tunaendelea makala hiyo ambapo tutazungumzia masuala ambayo mpenzi wako anapaswa kuwa nayo, akiyakosa jua wazi kwamba hakufai.

Unachotakiwa kufanya ni kusajili mapenzi yenye malengo yanayotekelezeka. Unapomaliza kumchunguza kwa kina mwenzi wako ni muhimu kutengeneza mwongozo wa mapenzi yenu. Hampaswi kuwa kama wanyama, lazima mipango ya wapi mmetoka, mlipo na mnapoelekea izungumzwe na wote wawili, ukiona mwenzio anakukwepa ujue hakutaki.

Hata hivyo, watalaamu wa masuala ya mapenzi wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja anapaswa kumuona mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu, hayo ndio mapenzi ya dhati.

Ni vema kuwashirikisha ndugu zako pindi unapopata mwenza ili kuwapa nafasi na wao kuamua kama mapenzi hayo ni ya heri ama la. Wengi huwa wanapuuza hili kwa sababu wanakuwa hawana nia njema na wenzao.

Ndugu ana nafasi kubwa mno katika uhusiano wako, kwani anaweza kuwa ngao ya kulifanya penzi lenu kuwa imara. Kama mwenzio haoni haja ya kukuweka karibu na ndugu zake, jua wazi kwamba huyo hakufai.

Kama wapenzi mmeweza kujizuia kwa muda mrefu kufanya mapenzi kabla ya ndoa kwa makubaliano kwamba mtafanya hivyo mara baada ya kuona, ikitokea mmoja kachoka kusubiri na bado hajawa tayari kuoa/kuolewa, ni muhimu kujadiliana kuhusu hilo na kuamua kwa pamoja.

Ikitokea mmoja hataki kumsikiliza mwenzie jua wazi kwamba hana nia njema na wewe, kwani katika kuamua kufanya tendo la ndoa ni muhimu kuzingatia afya yako kwanza na mengine yatafuata.

Huwezi kumpenda mtu halafu usimsikilize, mapenzi ya kweli ni yale ya kusikilizana.
Kutimiza ahadi ya kuoana ni hatua muhimu ambayo watu wengi hushindwa kuitekeleza, hasa wale malaghai wa mapenzi.

Utakuta mtu anakuahidi kuwa mtafunga ndoa, wakati ukifika anakuzungusha na baadaye unasikia mwenzio ameshaoa/kuolewa. Hii huwa inaumiza mno hivyo ni vema kuwa makini na matapeli wa mapenzi.

Masuala ya mapenzi ni magumu mno kama hakutakuwapo umakini wa kuchagua. Kinachotakiwa kila mmoja wetu awe na chaguo sahihi ili kuepuka kuambukizana maradhi na kuzaa watoto ovyo hatimaye kuwatelekeza.

Matokeo ya kuishia kwenye mikono ya walaghai ni kupata maradhi kwa kuwa ni lazima mwenzio atakuwa anahangaika na wengine huko mitaani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles