27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

UKILA ZABIBU MARA KWA MARA HUTAUGUA BAWASILI

Na HERIETH FAUSTINE,

ZABIBU ni matunda matamu yanayopendwa na watu wengi. Matunda haya yana faida nyingi kiafya katika mwili wa binadamu.

Matunda haya yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana zaidi mkoani Dodoma.

Zabibu huwa na rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza, njano, kijani na hata pinki,

Pia hutumika katika kutengeneza mvinyo (wine) ambayo hutumiwa katika sehemu mbalimbali duniani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), linaeleza kuwa asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengenezea mvinyo na asilimia 27 huliwa kama matunda ya kawaida, huku asilimia mbili ikikaushwa.

Licha ya kuwa ni tunda linalopendwa, pia linasaidia kupunguza uchovu na kuzuia mtoto wa jicho.

Zabibu ni tiba tosha ya pumu, huongeza unyevuvyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza utokeaji wa pumu.

Pia huimarisha mishipa kutokana na kuwa na madini ya shaba, chuma na manganizi ambayo huifanya mifupa kuwa imara na yenye afya.

Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuifanya isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo mtumiaji hupunguza hatari ya kupata kiharusi.

Zabibu pia zina viondoa sumu (antioxidants) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo na  hupunguza tindikali ya uriki (uric acid) kwa kuongeza kiasi cha mkojo unaotengenezwa na figo.

Vile vile zabibu zilizokaushwa zina faida nyingi pia kama kuzuia choo kigumu, homa na kuongeza damu.

Tunda hili pia husifika kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususani kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili.

Hali kadhalika zabibu pia husaidia katika tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Aidha, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi kwa ufasaha zaidi na kuzuia ukavu wa haja kubwa.

Lakini pia, madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles