29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ukawa wamponda Sitta kumwachia mkewe jimbo

Samuel-SittaElias Msuya,Tabora

MSAFARA wa mgombea mwenza wa urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Juma Duni Haji, juzi uliingia katika Jimbo la Urambo mkoani Tabora, huku makada wa umoja huo wakimponda mbunge wa jimbo hilo aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta, kwa kumwachia mkewe, Margaret Sitta kugombea jimbo hilo.

Sitta ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi, amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa muda mrefu, huku mkewe akiwa mbunge wa viti maalumu.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Mwananchi Square, Mratibu wa Kanda ya Kaskazini, Nicolas Ngowi, alisema kama Sitta ameshindwa kuliletea maendeleo jimbo hilo, mkewe pia hataweza.

“Jimbo hili linaongozwa na wabunge wawili wanaoishi nyumba moja, wanaoga pamoja, wanalala pamoja, lakini jimbo halina maji. “Urambo inaongoza kwa umasikini, watoto wanaota sugu kwenye makalio kwa kukaa chini. Walikuwa mke na mume wameshindwa kutatua kero, Mama Sitta ataweza?” alisema Ngowi.

Aliwataka wananchi wa Urambo Mashariki kutorubuniwa na zawadi za Mama Sitta kwa kuwa si za kudumu.

“Amesema atawanunulia vijana bodaboda kwenye kata 18, pikipiki 18, nani ataendesha? Anasema atanunua cherehani tano kwenye jimbo lenye wanawake zaidi ya 65, nani atashonea? Ule wakati wa kukamata kuku kwa kurushia punje za mahindi umekwisha. Hivi ninyi thamani yenu ni baiskeli?” alihoji Ngowi akishangiliwa na wananchi waliofurika katika uwanja huo, huku baadhi ya wakishika mabango yaliyoandikwa ‘Urambo siyo ya mke na mume’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles