28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

UKAWA KUTOA MSIMAMO KUHUSU UCHAGUZI MDOGO LEO

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), leo vinatarajiwa kutoa msimamo  endapo vitashiriki uchaguzi mdogo wa majimbo matatu Januari mwakani. Vyama hivyo vitatu ni Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi,

Majimbo hayo   ni   Songea Mjini (Ruvuma), Singida Kaskazini (Singida) na Longido mkoani Arusha.

Taarifa za awali ambazo MTANZANIA ilizipata zilieleza kuwa vyama hivyo vinatafakari kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo kwa kile vinachodai kuwa demokrasia inaminywa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo,   vyama hivyo vya upinzani vilisononeshwa na uchaguzi  wa marudio wa madiwani uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita kwa kile vilichodai  ulitawaliwa na ubabe wa polisi.

Katika taarifa yake   jana, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema vyama hivyo vitazungumza   na   waandishi wa habari kujadili mustakabali wa masuala muhimu ndani ya nchi hususan mwenendo wa siasa.

Hata hivyo, mkutano huo ambao ulipangwa kufanyika jana katika hoteli ya Colosseum   Oysterbay,   Dar es Salaam, uliahirishwa ghafla.

Hiyo ni mara ya pili kuahirishwa  mkutano na waandishi wa habari.  Juzi Chadema ilitoa mwaliko kwa vyombo vya habari kwamba kingetoa taarifa kuhusiana na maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichomalizika hivi karibuni.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu aliwaambia waandishi wa habari  waliofika katika hoteli hiyo kwa ajili ya mkutano huo jana  kuwa mkutano hulo uliahirisha kwa kuwa majadiliano yalikuwa hayajakamilika.

“Tunaomba mtuwie radhi, kuna maazimio ambayo tuliyafikia lakini kuna wenzetu wamechelewa hatujawa-brief, hivyo muda huu tunarudi kwenye kikao ili tuwa-brief.

“Tukisema muondoke halafu mrudi baadaye tutakuwa tunawasumbua, tunaomba tukutane kesho (leo) kwa ajili ya mkutano huo,”alisema Mwalimu.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles