25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

UKATA WAKWAMISHA USAJILI YANGA, YONDANI, KAKOLANYA WAWEKA MGOMO

 

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema hategemei kufanya usajili wowote katika dirisha dogo lililofunguliwa rasmi Novemba 15 kutokana na klabu hiyo kuyumba kiuchumi.

Zahera amesema ukata huo unaoikabili timu hiyo yenye maskani yak mitaa ya Jangwani imesababisha wachezaji wao wawili kugoma kusafiri na timu kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui ya Shinyanga.

“Nimefika Shinyanga salama na mambo yako vizuri kwa nguvu za mwenyezi Mungu lakini nimepewa taarifa kuwa mlinda mlango, Beno Kakolanya na beki, Kelvin Yondani wamegoma kusafiri na timu kutokana na kukosa mishahara wa miezi mitano wanayoidai klabu hiyo,” amefafanua Zahera.

Amesema kutokana na timu hiyo kukabiliwa na ukata hatoweza kusajili kwenye dirisha dogo licha ya mashabiki na wadau wa timu hiyo kuwa na matumaini ya kufanya usajili mzuri na wenye tija kubwa kwa timu hiyo.

“Najua wote mnasubiri kuniuliza baada ya dirisha dogo kufunguliwa kama kuna mchezaji nitakayemsajili, nachotaka kuwaambia ni kuwa kupata mchezaji kunahitaji pesa za kumtoa katika klabu aliyopo pia kuna makubaliano ya mshahara na mimi sioni kama vitu vyote hivyo tunaweza kuvikabili,

“Kuna viongozi wengine wameniambia nitafute wachezaji, sasa mimi nitamweleza nini huyo mchezaji wakati timu haiwezi kufuata masharti ya uhamisho wa mchezaji, ninachokiona hapa tutaendelea na wachezaji hawa tulio nao,” ameeleza zaidi kocha huyo anayeifundisha pia timu ya Taifa ya Congo akiwa kocha msaidiki.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles