23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Ukarabati Mv Nyerere kugharimu Sh milioni 50

BENJAMIN MASESE-MWANZA

SERIKALI imetenga Sh milioni 50 katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya ukarabati wa kivuko cha Mv Nyerere kilichopinduka Septemba 20, mwaka jana wakati kikisafirisha abiria kutoka Bugorola kwenda Ukara wilayani Ukerewe na kusababisha watu 230 kufariki dunia na wengine 41 kunusurika.

Pia imetenga Sh bilioni tano kwa ajili ya  ukarabati na kununua vivuko pale inapohitajika ikiwa lengo ni kuimarisha na kuwaondolea adha wananchi wanaovuka  au kuishi katika maeneo ya visiwani.

Akizungumza jijini hapa juzi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (Temesa), Japhet Masele, alisema wametenga fedha hizo ambazo ni mapato ya ndani kwa lengo la kukarabati vivuko na hata kuvinunua pale inapohitajika.

Alisema mbali ya fedha za mapato ya ndani, Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa Temesa pale panapojitokeza kuwapo na shughuli ya ujenzi wa kivuko kipya au ukarabati ikiwa lengo ni kuondoa changamoto za vyombo vya kusafirisha abiria na mizigo majini.

“Mfano kwa sasa Serikali imetoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa kivuko cha Mv Nyerere ambacho kilipinduka Septemba 20, mwaka jana, pia imetoa shilingi milioni 10 nyingine kwa ajili ya ukarabati wa vivuko mbalimbali ambavyo vilikuwa na kasoro.

“Tunaposema tumetenga shilingi bilioni tano kama fedha za ndani, tayari tumepanga kutengeneza boti mbili mpya na moja itapelekwa katika Kisiwa cha Ilugwa na nyingine tutaangalia palipo na uhitaji wa haraka, kama Serikali tunatambua uwepo wa vivuko unaongeza uchumi kwa wananchi.

“Vipo vivuko ambavyo vinaziunganisha nchi za EAC, mfano kivuko cha Kigongo-Busisi ambacho kwanza kinaunganisha mkoa na mkoa, pia kinatumiwa na nchi za nje. Vile vile Kivuko cha Rusumo nacho kinatumika kwa EAC ambapo vyote vinavusha malori ya mafuta,” alisema.

Pia alisema muda wowote, Serikali itasaini mkataba wa ujenzi wa kivuko kipya cha Bugorola-Ukara kitakachokuwa mbadala wa Mv Nyerere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles