24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ukaguzi leseni na vyeti vya madereva waanza

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga
Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga

ADAM MKWEPU NA CHRISANTA CHRISTIAN, DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi jana limeanza kufanya ukaguzi wa leseni na vyeti vya madereva kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani na nchi jirani Ubungo (UBT), jijini Dar es Salaam kufuatia ajali za barabarani nchini kuongezeka.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alisema kuwa ukaguzi huo una lengo la kuchunguza madereva ambao wanafanya shughuli hizo kinyume na sheria na kusababisha kuwapo kwa ajali nyingi za barabarani.

“Lengo letu ni kuhakikisha madereva wanakuwa na vyeti pamoja na leseni halali. Hakuna atakayeachwa katika zoezi hili kwa sababu linaendeshwa katika mikoa yote ambayo mabasi makubwa yanasafiri ili kuepusha ubabaishaji wa madereva,” alisema.

Kuhusu malalamiko ya kuwapo urasimu katika zoezi hilo, Kamanda Mpinga alisema hata kama dereva hatakaguliwa katika kituo  cha Ubungo, atakwenda kukaguliwa mikoani ili kufanikisha zoezi hilo.

Umoja wa Madereva wa Mabasi (UWAMATA), ulilalamikia kuwapo kwa urasimu katika zoezi hilo kwa madai kuwa madereva wengi hawajakaguliwa.

Mmoja wa wajumbe wa umoja huo, Jabu Chagenya, alisema serikali inapaswa kuwa na nia ya dhati katika kupambana na tatizo hilo na kuacha kutimiza majukumu yake kisiasa.

“Huwezi kufanya ukaguzi wa aina hii kwa kuuliza namba ya leseni pamoja na kuhoji cheti, ingepaswa kuwapo kwa ushirikishwaji wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kutambua vyeti hivyo kama ni feki.

“Kilichotokea ni usumbufu kwa abiria na kama wataendelea kufanya ukaguzi kwa mtindo huu sidhani kama utakuwa na mafanikio kwa kuwa watu ambao tunajua matatizo ya madereva hatushirikishwi,” alisema Chagenya.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Ninakubali kuwa ukaguzi huu wa leseni unafanywa chini ya kiwango hali ambayo inasababisha usumbufu kwa habiria. Mfano badala ya wakaguzi kutafuta muda muhafa wa kufanya ukaguzi wao wanafanya ukaguzi huo saa 12 asubuhi wakati habiria tayari wakiwa katika magari tayari kwa kusafiri. Jana Alhmisi tarehe 11.09. 2014 nilibaini hali hii hali ambayo ilinifanya nipate wazo kuwa hata askari wa usalama barabarani hawana takwimu za mabasi ya habiria waendao mikoani na wala takwimu za madereva wa mabasi hayo. Jambo hili ni kosa na ndilo linalosababisha ukaguzi kufanyika muda ambao si muhafaka. Hivyo, ni vyema kitengo cha polisi cha Usalama Barabarani kikawa na tawimu za mabasi ya mikoani na madereva wa mabasi hayo tena takwimu za mara kwa mara hili ziwasaidie katika ukaguzi siyo kuvamia mabasi asubuhi saa 12 na kuanza ukaguzi wakati habiria wanataka kusafiri. Kama ukaguzi kwa mtindo huu utaendelea ni bora habiria wawe wanalipwa fidia ya usumbufu maana wao si sehemu ya maslahi ya madereva hao wanaokaguliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles