29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

UJUMBE WA UN WAWASILI MYANMAR KUCHUNGUZA MATESO YA WAROHINGYA

RANGOON, MYANMAR


UJUMBE wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) unaochunguza mzozo wa Myanmar kuhusu Warohingya umewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo jana.

Jopo hilo linatembelea nchi hii jirani na Bangladesh ambako Warohingya 700,000 waliokimbia ghasia zinazoongozwa na Jeshi la Myanmar wanaishi katika kambi ya wakimbizi.

Ujumbe huo ulio katika ziara ya siku mbili, jana ulitarajia kukutana na Kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi na Kiongozi wa Jeshi Min Aung Hlaing.

Na leo utatembelea jimbo la kaskazini la Rakhine ambalo Warohingya walilikimbia.

Wakiwa huko watajionea athari za operesheni ya kijeshi na kutathmini maandalizi ya Serikali ya Myanmar ya kuwapokea Warohingya watakaorejea kutoka Bangladesh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles