27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

UJUMBE WA DK. MSELI KWA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI

NAOMBA kujitambulisha kama Mtanzania, nilizaliwa mwaka 1958, Ndungu, Same, mkoani Kilimanjaro. Nilimaliza Shahada yangu ya Uzamili (Master of Science in Engineering) upande wa Sayansi ya Upembuzi wa Chuma “extractive of ferrous metals” Sofia, Bulgaria mwaka 1989. 

Baada ya hapo, kwa juhudi zangu mwenyewe, nilielekea Sweden katika Chuo cha Royal Institute of Technology (KTH) na mwaka 1999 nilipata Shahada ya Uzamivu (PhD). Tafiti zangu zilihusu Experimental and Modelling of the Refining Capability of Metallurgical Slags. Ukiangalia www.google.com utaona tafiti zangu zote (25+) na zinatambulika kimataifa. Slag ni jina linatumika likiimanisha hifadhi ya uchafu wote, katika upembuzi chuma. 

Kuanzia mwaka 1999 mpaka sasa mie ni Mtafiti Mwandamizi, Utafiti na Maendeleo (Research and Development (R &D)) katika kiwanda cha vyuma cha kutengeneza vyuma special (tool steels),  Uddeholms AB. Majukumu yangu ni uangalizi na utekelezaji wa utafiti na maendeleo majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja
• muda mrefu utafiti na maendeleo (ndani ya Uddeholms AB na nje ya Uddeholms AB)

• muda mfupi utafiti na maendeleo (ndani ya Uddeholms AB).

 

Ni majukumu mapana ambayo yananihusisha kushughulikia na utafiti unaouhusisha mitandao mikubwa ya ushirikiano ndani ya Sweden na nje ya Sweden. Haya majukumu yamenipa fursa ya kuzungumza na mtandao wa watu mbali mbali na kupata maarifa tajiri.

 

Ujumbe wangu kwa Watanzania wanaoishi Ughaibuni

Ni kujaribu kuwa mfano wa kuigwa (Role Model). Nimejaribu kuepuka kutumia neno Diaspora kwa sababu sijajua mpaka sasa Tanzania inamaanisha nini ikitumia neno Diaspora.

Tafsiri niijuayo mimi ni kikundi chochote ambacho kimetawanywa nje ya nyumbani kwao (nchini kwao) hasa kwa kutokupenda (involuntarily), kama Waafrika walivyotawanywa wakati wa Trans-Atlantic biashara ya watumwa.

Marekani wana tafsiri nyingine na Wayahudi/Waarabu wana tafsiri tofauti. Swali langu kuanzia 1999 nafanya kazi hapa Sweden kama mtaalamu na kuanzia nizaliwe mwaka 1958 sijabadilisha uraia na ni Mtanzania; Je mimi ni Diaspora? Hii ndio sababu ambayo imenifanya niepuke kutumia neno Diaspora na badala yake kutumia Watanzania wanaoishi Ughaibuni.

Hawa “Diasporas” ni watu ambao viongozi wetu huwa wanawalilia  walete  ukwasi wao ili kujenga maendeleo Tanzania.  Ni hotuba nimezisikia kwa viongozi hutoa mbele ya Wazungu. Viongozi wetu wakija ni lazima watamke neno 'Diaspora' mbele ya Wazungu kuonyesha jinsi “Diaspora” wa Tanzania wanavyoweza kuchangia maendeleo ya Tanzania. Katika kumbukumbu zangu sijaona matamshi yakitekelezwa.

Viongozi wetu wakitamka jinsi “Diaspora” wa Tanzania wanavyoweza kuchangia maendeleo ya Tanzanai, wana maana “Diaspora” kuwekeza Tanzania, uwekezaji binafsi. Uwekezaji binafsi unahitaji hela; ila labda viongozi wetu wamesahau uwekezaji wa maarifa. Elimu tuliyopata Ughaibuni kuisambaza Tanzania ili kuchangia katika maendeleo ya Tanzania. Huu ndio Ujumbe wangu kwa Watanzania wanaoishi Ughaibuni au Diaspora au mtaalamu anayeishi Ughaibuni.

Tunajaribu kuwa mifano ya kuigwa (Role Models), yaani, tuonyeshe tabia, mifano, au mafanikio ili uigwe na wengine na hasa vijana wa nchi yetu. Kama tukionyesha kuuza dawa za kulevya Ughaibuni ndio njia ya kupata mafanikio tutakuwa hatuwi mfano mzuri wa kuigwa, hasa vijana wa nchi yetu. Kama tukionyesha udanganyifu/utapeli wa taaluma zetu ndio njia ya kupata misaada toka serikalini au kuajiriwa tutakuwa hatuwi mfano mzuri wa kuigwa.

Mfano wangu binafsi wa kuigwa ulianza tokea 1996 nikiwa bado sijapata Shahada ya Uzamivu (PhD). Kuanzia hapo, kwa uamuzi wangu mwenyewe, nilionyesha nia yangu ya kusambaza taaluma ya Sayansi ya Malighafi (Material Science) Tanzania.

 

Hii ni baada ya kuona kwamba nchi yetu ina maliasili nyingi, ikiwa ni pamoja na madini rasilimali na nishati (gesi asilia). Kama sikosei Tanzania ina nia ya kuendeleza na kukuza sekta ya viwanda. Lakini, Tanzania inakabiliwa na idadi ya vikwazo ambavyo vinazuia sekta hii kuendelea na kukua. Mojawapo ni ukosefu wa wataalamu wajuao taaluma ya metallurgy. Hii inafanya Taifa kutoweza kutumia umuhimu wa madini katika kuboresha maisha ya Watanzania na kushindwa kupunguza umaskini. Nia yangu ni kuona Tanzania inaanzisha na kukuza maendeleo ya sekta ya metallurgical industry na hasa chuma ikiwa na lengo la kuzalisha metals kutoka kwenye madini yetu. 

 

Baada ya kupata fursa ya kutembelea sehemu ambazo madini yanapatikana, nimeona "viungo vinachokosekana" katika ushirikiano kati ya uchimbaji wa madini na bidhaa za uzalishaji. Umuhimu wa hizi "missing gaps" si rahisi kuzijua kama huna taaluma ya Sayansi ya Upembuzi wa Chuma Ni hizi "missing gaps"  nchi inapoteza nafasi ya kuongeza thamani ya malighafi (madini) kabla kuuza nje ya nchi na kupoteza nafasi ya kujenga ajira, hivyo kupunguza umaskini. Kwa mfano,

1. wataalamu wa uchimbaji madini tunao ila wataalamu usindikaji wa madini hatuna;  matokeo yake badala ya kuongeza thamani, tunauza nje ya nchi na kupoteza mapato ya Taifa

2.  Katika upembuzi wa chuma (uyeyushaji wa chuma chakavu); hakuna ujuzi wa kudhibiti ubora na matokeo yake ubora ambao haufikii viwango vya viwanda.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, alieleza kuhusu Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu. Mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa umepangwa uongezeke kutoka asilimia 5.7 mwaka 2015 na kufikia asilimia 5.8 mwaka 2020 na asilimia 5.9 mwaka 2025.

Wakati analizindua Bunge la 11, Rais Magufuli alieleza lengo lake ni kukuza sekta ya viwanda iweze kuajiri asilimia 40 ya nguvu kazi mwaka 2020. Ili mpango huu ufanikiwe ni lazima uchambuzi changamoto za kufikia lengo hili, ikiwa na changamoto za kujaza “missing gaps”.

Tukumbuke pia, wakati alipotembelea kwenye miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga alisema Serikali lazima ijiridhishe ni kwa namna gani itafaidika na uwekezaji katika miradi ya makaa ya mawe na chuma kabla haijaanza. Miradi hiyo inatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Ltd (SHG) ya China.

Alisema  “Madini haya yana viwango vya juu vya ubora, hivyo ni lazima tuwe makini kabla ya kuanza kwa uzalishaji wake. Kwani chuma chetu ni bora na tutachimba kwa zaidi ya miaka 50, hivyo maeneo haya ni nyeti na lazima Serikali ijipange vizuri na kujiridhisha kama vipengele vyote vya mkataba vimetengamaa ndipo mradi huo uanze,”.

Hivi karibuni, akitembelea mgodi wa Liganga, Ludewa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema Serikali lazima ijiridhishe ni kwa namna gani itafaidika na uwekezaji katika miradi ya makaa ya mawe na chuma kabla haijaanza. Alisema Serikali iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na mwwekezaji kabla ya kuanza uzalishaji kwenye miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.  Miradi hiyo inatekelezwa kwa ubia kati ya  Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Ltd (SHG) ya China.

Alisema “Madini haya yana viwango vya juu  vya ubora, hivyo ni lazima tuwe makini kabla ya kuanza kwa uzalishaji wake. Kwani chuma chetu ni bora na tutachimba kwa zaidi ya miaka 50,”. “Hivyo maeneo haya ni nyeti na lazima Serikali ijipange vizuri na kujiridhisha kama  vipengele vyote vya mkataba vimetengamaa ndipo mradi huo uanze,”.

Alisema, mradi huo hautachukua muda mrefu utaanza hivyo wananchi wawe na subira. “Hatutaki kusikia tena suala la mikataba mibovu tunataka mikataba itakayoleta tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles