27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

UJIO WANAFUNZI WA LUCKY VINCENT WAZUA FURAHA, SIMANZI

-Na MARGRETH MWANGAMBAKU , ANNASTAZIA MAGUHA

Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent, Doreen Mshana, Wilson Tarimo na Sadia Awadh wamerejea nchini wakitokea nchini Marekani walikokuwa wakitibiwa baada ya kupata ajali Mei 6, mwaka huu.

Wanafunzi hao waliwasili kati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA), saa 3:33 asubuhi leo Agosti 18, na kupokewa na viongozi wa kitaifa, walimu na wanafunzi wa shule hiyo na ndugu jamaa na marafiki ambapo ujio wao huo uliibua simanzi na furaha kwa watu wengi waliokuwapo uwanjani hapo kuwapokea.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan ambaye alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mughwira, pamoja na mambo mengine alilipongeza Shirika Good Samaritan kwa kuanzisha mfuko maalumu wa kuwasomesha watoto hao hadi chuo kikuu.

“Serikali inapenda kumwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoa Sh milioni 20 kutunisha mfuko huo fedha ambazo nimetaarifiwa ni miongoni mwa rambirambi zilizokuwa zimetolewa na wanajamii baada ya ajali kutokea.

“Sisi pia tungeweza kuwahudumia watoto wetu hapa lakini gharama zake zingekuwa tofauti, utunzaji wake ungekuwa tofauti, familia zingekaa pamoja na serikali ingepata nafasi ya kuwaona watoto kila wakati lakini kwa sababu ya mara nyingi ubadhirifu wetu na tabia ya ubinafsi tunashindwa kutunza rasilimali zetu kwa kushindwa kuokoa watoto watatu tu achilia mbali ajali zinazitokea kila siku kwa hali ya watu kutokujali,” amesema Mama Mughwira.

Katika tukio hilo, wanafunzi hao walipata nafasi ya kusalimia umati wa watu waliokuja kuwalaki uwanjani hapo na kuwashukuru hatua iliyoibua machozi ya furaha kwa watu mbalimbali uwanjani hapo huku baadhi ya wazazi wakilia kwa simanzi kwa kupoteza watoto wao waliofariki katika ajali hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles