25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

UJIO WA LACAZETTE HAUNA MAANA AKIONDOKA OZIL, SANCHEZ

NA BADI MCHOMOLO



MASHABIKI wa klabi ya Arsenal wamekuwa na furaha kubwa baada ya kuona kocha wa timu hiyo Arsene Wenger ameweza kumalizana na aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Lyon, Alexandre Lacazette.

Mshambuliaji huyo amejiunga kwa kitita cha pauni milioni 53, ambazo ni zaidi ya bilioni 151 za Kitanzania. Imani kubwa kwa Arsenal ni kwamba mchezaji huyo anakuja kufuta janga la kukosa mataji kwenye uwanja wa Emirates.

Kutokana na uwezo wake wa ushambuliaji ni wazi kwamba anaweza kutoa mchango mkubwa sana katika ushindi wa klabu hiyo, kazi yake imeonekana akiwa na Lyon ambapo aliweza kupambana na kufunga aina mbalimbali ya mabao hata kwenye mazingira magumu.

Msimu uliomalizika hivi karibuni Arsenal iliandika historia mpya ya kuwa nje ya nafasi nne katika msimamo wa Ligi nchini England, ikiwa ni mara yao ya kwanza kushika nafasi chini ya nne kwa miaka 20. Msimu huo uliomalizika hivi karibuni ilimaliza nafasi ya tano.

Japokuwa iliweza kumaliza nafasi hiyo lakini mchango mkubwa ulitokana na wachezaji wao Mesut Ozil, Aleix Sanchez na wengine, lakini wawili hao walikuwa na mchango mkubwa zaidi, bila ya hivyo kuliwa na uwezekano kwamba klabu hiyo ingemaliza chini ya nafasi ya tano.

Arsenal ilikosa namba tisa tegemeo, Sanchez hakuja Arsenal kucheza namba tisa, ila alijiunga na kikosi hicho kwa ajili ya kucheza nafasi ya ushambuliaji wa pembeni, lakini kutokana na mshambuliaji wao Olivier Giroud kucheza chini ya kiwango, Wenger aliamua kumbadisha Sanchez na kumfanya acheze namba hiyo ya Giroud.

Sanchez alijitahidi kuonesha uwezo wake katika nafasi hiyo huku Ozil akicheza nyuma yake kwa ajili ya kumpigia pasi za mwisho au akitokea pembeni ili kuongeza mashambulizi, wawili hao waliweza kutengeneza umoja na kuifanya Arsenal kuwa na mvuto mkubwa nyota au wakiwa uwanjani.

Kwa sasa Arsenal inaonekana kushindwa kukaa vizuri na wachezaji hao wawili ambao wameomba kupandishiwa mshahara ili waendelee kubaki katika kikosi hicho. Wapo tayari kuondoka katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji ili kutafuta sehemu nyingine ambayo itakuwa na manufaa kwao.

Wenger baada ya kuona wachezaji hao wapo kwenye mipango ya kuondoka akaamua kuinasa saini ya Lacazette. Wenger yupo sahihi kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao, lakini hayupo sahihi kuwaacha Ozil na Sanchez wakiondoka.

Kazi iliobaki kwa Wenger sasa ni kuhakikisha anaweza kuwazuia wachezaji hao wawili wasiondoke, hivyo anatakiwa kuwaboreshea mikataba yao waweze kutengeneza kikosi cha kupigania mataji.

Itakuwa kazi rahisi sana kwa Lacazette kucheka na nyavu mara kwa mara kwa kuwa, Ozil atacheza nafasi yake ya mshambuliaji wa pembeni au atasimama nyuma ya namba tisa ili kumpigia pasi za mwisho, huku Sanchez akicheza kwa kujidai katika nafasi yake ya pembeni.

Sio kosa kubwa kumuacha Giroud akiondoka katika kipindi hiki cha majira ya joto na kumpisha Lacazette ambaye anaonekana kuwa na makali, lakini sio kuwaacha Ozil na Sanchez wakiondoka, litakuwa kosa kubwa sana.

Hakuna sababu kubwa sana ya kuvunja beki ili kuitafuta saini ya kiungo wa Monaco, Thomas Lemar na mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez, lakini kama bajeti ya usajili msimu huu inatosha sio mbaya kuwaongeza wachezaji hao.

Watalaamu wanajaribu kumshauri Wenger kwamba ni bora akamuacha Giroud aondoke kutokana na mchango wake kuwa mdogo baada ya kucheza jumla ya michezo 29 msimu wote katika kikosi cha Arsenal na kufunga mabao 12, wakati huo usajili mpya wa Lacazette akicheza michezo 30 ndani ya Lyon na kufunga mabao 28.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles