28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ujio wa Kenyatta wamkuna Magufuli, awakaribisha wawekezaji kutoka Kenya

Bethsheba Wambura

Rais Dk. John Magufuli amesema amefurahishwa na ujio Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta hapa nchini na amempongeza kwa kuwa Rais wa kwanza wa nje kutembelea Wilaya ya Chato.

Amesema ukiachilia mbali ujirani uliopo baina ya Tanzania na Kenya, pia kuna undugu kwa kuwa wananachi wake wanazungumza lugha moja, na muingiliano wa kijamii ikiwamo kuoana na utamaduni unaofanana.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Julai 5, alipokuwa akizungumza baada ya kumpokea mgeni wake Rais Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Chato kwa ziara binafsi ya siku mbili hapa nchini.

“Kufika kwako hapa Chato umeudhihirishia umma wa dunia kuwa sisi ni majirani, na marafiki wa kweli siku zote tutatembea pamoja kamwe tusikubali kulaghaiwa na watu,” amesema Rais Magufuli.

Amesema kutokana na ushirikiano huo wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii ikiwamo kuwekeza katika nchi hizo mbili.

“Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kenya imewekeza miradi 504 yenye thamani ya dola za marekani bilioni 1.7  ikiwa na idadi ya watu 50,956 huku wawekezaji wa Tanzania nchini Kenya wakiwa 24.

“Na katika sekta ya utalii, Tanzania ni nchi ya pili kwa watu wake kutembela Kenya ikitanguliwa na Marekani ambapo kwa mujibu ya takwimu za Bodi ya utalii ya Kenya ya mwaka 2018 Watanzania 222, 216 walitembelea Kenya ambayo ni zaidi ya asilimia 10 ya watu wote waliotembelea Kenya.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameitaja miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kwa ushirikiano wa nchi hizi mbili ikiwamo barabara ya Holili- Arusha hadi Namanga pamoja na maandalizi ya ujenzi wa barabara kutoka Mombasa hadi Bagamoyo.

Vile vile Rais Dkt. Magufuli ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Kenya kuja kuwekeza nchini hapa kwa kuwa milango ipo wazi kwa mwekezaji yeyote na Watanzania waendelee kuwekeza Kenya ili kuendeleza ushirikiano uliopo kwa mustakabari wa maendeleo ya nchi zote mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles