24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ujerumani yatangaza maambukizi mapya 16,000 ya corona ndani ya siku moja

BERLIN, UJERUMANI

MAAMBUKIZI mapya 16,774 ya virusi vya corona yameripotiwa nchini Ujerumani ndani ya siku moja. 

Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani ya Robert Koch ikinukuu taarifa kutoka mamlaka za afya, imesema watu hao walithibitishwa kupata maambukizi hayo jana.

Maambukizi hayo mapya yametangazwa siku moja tu baada ya watu wengine 14,964 kurekodiwa kupata maambukizi hayo juzi. 

Jana, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alitetea hatua kali mpya zilizotangazwa na Serikali yake kupambana dhidi ya virusi vya corona, akionya kwamba propaganda zinahujumu juhudi hizo.

 “Acha niwe muwazi, habari za uwongo, kula njama na chuki sio tu zinaharibu mijadala ya kidemokrasia, bali pia vita dhidi ya virusi vya corona,” alisema Merkel. 

Tangu kuanza kwa janga hilo, jumla ya watu waliothibitiswa kuambukizwa virusi hivyo nchini Ujerumani imefikia 481,013, huku vifo vinavyohusiana na maambukizi hayo vimefika 10,272.

UFARANSA

Nchini Ufaransa, hatua kali mpya za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona zilizotangazwa, zinaweza kuongezewa muda zaidi ya tarehe ya mwisho ya Desemba mosi.

Hayo ni kwa mujibu wa mshauri wa Serikali wa masuala ya kisayansi, Profesa Jean-François Delfraissy. 

Rais Emmanuel Macron alisema jana kwamba Ufaransa huenda ikaanza kupunguza vikwazo hivyo pale maambukizi ya virusi vya corona yatakapoanza kupungua na kufikia 5,000 kwa siku badala ya idadi ya hivi sasa ya maambukizi 40,000 kwa siku moja. 

Lakini Delfraissy alisema haamini kama hilo linaweza kufanikiwa ifikapo Desemba mosi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles