27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Ujerumani yajitosa mgogoro wa Sudan

BERLIN, Ujerumani

SERIKALI ya hapa  imesema ina matumaini ya kufanyika uchaguzi huru nchini Sudan na imeuwasilisha mgogoro wa nchi hiyo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN).

Hata hivyo serikali hiyo imesisitiza kuwa Omar al-Bashir afikishwe kwenye mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).

Katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Christopher Burger aliweka tahadhari wakati alipoisoma taarifa rasmi juu ya hali inayobadilika kwa haraka na isiyotabirika ya nchini Sudan.

Msemaji huyo alisema jambo la uhakika ni kwamba Aprili 11 mwaka huu, jeshi katika jiji la Khartoum lilichukua udhibiti wa kituo cha televisheni cha taifa na kutangaza litatoa tamko baadaye juu ya hali ya kisiasa ya Sudan na na kwamba Rais wa muda mrefu Omar al-Bashir ameondolewa madarakani.

Hata hivyo, watu wengi waliingia mabarabarani mwishoni mwa wiki  usiku ili kuendelea kuonyesha kwamba wanataka jamii huru, demokrasia na nchi itayoongozwa na serikali ya kiraia.

Msemaji huyo   alitoa wito kwa pande zote zijizuie kwa sababu ufumbuzi wa amani katika mgogoro huo unahitajika na pia utakaozingatia matarajio ya watu wa Sudan wanaotaka mabadiliko.

Burger alisema Ujerumani, ambayo mwezi huu inashikilia urais wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imeupa kipaumbele mgogoro wa Sudan kati ya ya ajenda zitakazojadiliwa pamoja na washirika wake wa Ulaya na Marekani.

Alhamisi wiki iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa tahadhari juu ya hali katika nchi hiyo ya Mashariki mwa Afrika na iliandikwa kwenye tovuti yake kwamba Usafiri wote usio muhimu kwenda nchini Sudan unapaswa kuepukwa, na viwanja vya ndege na mipaka kwa sasa imefungwa.

Mpaka sasa haijulikani bado alipo Rais Al Bashir lakini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameeleza kuwa msimamo wa Ujerumani upo wazi kwamba hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo  iliyotolewa na ICC kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur bado ina nguvu.

Rais Bashir mwenye umri wa miaka 75 anatuhumiwa kwa kuwatumia askari na jeshi lake kuyasakama kikatili makundi ya wachache huko Darfur Magharibi mwa Sudan mnamo mwaka 2003.

Inakadiriwa watu 300,000 waliuawa katika vita hivyo. Uongozi mpya wa kijeshi wa nchini Sudan umesema al-Bashir atafunguliwa mashtaka nchini na siyo nje ya Sudan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,894FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles