29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Ujenzi wa Reli ya SGR Dodoma-Tabora waanza

Na Allan Vicent, Tabora

MRADI wa ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway-SGR) kutoka Makutupora jijini Dodoma kuja Mkoani Tabora umeanza rasmi baada ya Mkandarasi Kampuni ya Yapi Merkez ya nchini Uturuki kusaini mkataba na kupewa baraka zote ili kuanza kazi hiyo. 

Akizungumza jana baada ya kusaini mkataba huo katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Hotel ya JM mkoani hapa Mhandisi Mshauri Chedi Masambaji alisema mradi huo utatekelezwa kwa weledi na kasi na utakamilika ndani ya muda wa miezi 46 kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.

Amesema mradi huo licha ya kuwa na Mkandarasi Mkuu pia kutakuwa na wahandasi wabobezi wa masuala ya ujenzi wa njia za reli kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi  pamoja na wachumi kutoka serikali kuu.

Mhandisi wa njia za Reli kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) Christopher Mwangwela alisema mkataba huo uliotiwa saini kati ya serikali, Shirika la Reli na Kamapuni ya Yapi Merkez utekelezaji wake umeanza rasmi.

Alibainisha kuwa reli hiyo itapitia kusini mwa uwanja cha ndege wa Tabora kuelekea Wilaya ya Uyui karibu na Chuo cha VETA na hapo kutajengwa karakana kubwa kwa ajili ya shughuli za mradi.

Alifafanua kuwa reli hiyo itakuwa na jumla ya urefu wa kilomita 368 zikiwemo kilomita 294 za njia kuu na kilomita 74 za mchepuko.

Mchumi Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Albert Cheli alisema kupitia mradi huo wanatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 8,000 katika nyanja mbalimbali watakaofanyakazi katika chini ya  mradi huo mkubwa .

Aliongeza kuwa ajira hizo zitatolewa kwenye maeneo mradi utakapopita hasa maeneo ya Makutopora, Itigi, Manyoni na Tabora ambapo kwa Mkoa  wa Tabora pekee utaajiri ajira mbalimbali zaidi ya watu 2000  wataonufaika  .

 Meneja mradi kutoka kampuni ya Yapi Merkez,Hakani  Alkan ambaye aliwasilisha mpango kazi wake  alisema kuwa atakamilisha ujenzi wa mradi huo kwa muda wa  miezi 46 kama ilivyo kwenye mkataba

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles