28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ujenzi wa Nyumba za Wananchi waliokumbwa na mafuriko Hanang wafika hatua nzuri

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama, amewapongeza SUMA JKT kwa hatua nzuri waliyoifikia katika ujenzi wa nyumba za makazi kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mawe na matope mwezi Desemba mwaka jana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama akizungumza mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za wanachi waliokumbwa na maafa ya Maporomoko ya Matope na mMawe Hanang’ Desemba mwaka Jana.

Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo katika eneo la Waret, Kijiji cha Gidagamowd, Kata ya Mogitu, Wilaya ya Hanang’, leo tarehe 2 Julai 2024.

Ujenzi wa nyumba hizi ni kielelezo cha dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya uzalendo kwa taifa lake, utu, na mapenzi kwa wananchi katika kuwatumikia.

“Nimefurahi kuona mmehamasisha ujuzi wa ujenzi kwa sababu nyumba hizi zimejengwa kwa ubora wa hali ya juu na kuzingatia kanuni za kiuhandisi,” alisema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama alielekeza uongozi wa Mkoa wa Manyara kuhakikisha miundombinu ya elimu, soko, na afya inakamilika kwa muda unaotakiwa kama ilivyofanywa katika urejeshaji wa hali kwa kuhakikisha huduma za maji na nishati ya umeme zinapatikana sambamba na ufunguaji wa barabara.

Waziri Mhagama alisema, “Makazi yanapendeza na baada ya muda mji huu utakuwa mkubwa sana na utakuwa mji wa kihistoria. Ni vyema tukaendelea kutunza mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Hanang’, Mhe. Halimish Issa Hazali, alisema Waziri Mhagama ametembelea nyumba za SUMA JKT zipatazo 73 na nyumba 1 ya UWT, na ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi. Pia alitembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba 35 zinazosimamiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu.

“Ninamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na anaendelea kuifanya kwa wananchi wa Hanang’,” alisema Hazali.

Awali, Kaimu Kamanda wa Ujenzi wa Nyumba, Luteni Kanali Ashiraf Hassan, alisema wamefarijika na ziara ya Waziri Mhagama na wamejipanga kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

“Hatuwezi kumuangusha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika adhima yake ya kuhakikisha anawapatia wananchi wa Hanang’ waliokumbwa na mafuriko ya matope na mawe nyumba bora,” alisema Luteni Kanali Hassan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles