25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ujenzi reli ya kisasa washika kasi -Dk. Abbas

Ramadhan Hassan-Dodoma

MSEMAJI Mkuu wa Serikali,Dk.Hassan Abbas  amesema ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa  (SGR) kutoka Dar es Salaam – Morogoro, unaendelea kwa kasi na haujasimama kama ambavyo wanasiasa  wanadai.

Alisema mpaka sasa fedha zipo za kutosha kwa ajili ya kumalizia mradi huo.

Alisema mwaka huu, Watanzania kwa mara ya kwanza watapanda treni ya umeme.

Dk.Abbas, alitoa kauli hiyo  jijini Dodoma jana, alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema mradi huo,unaendelea kwa kasi na hakuna sehemu ambayo umesimama.

 “Ukisema reli imesimama, ninyi mpo Dodoma nendeni hata Ihumwa nendeni mkaangalie kama kuna eneo mradi umesimama hatuja wahi kukosa fedha, mradi unaendelea. 

“Hakuna hoja ya msingi mradi unaendelea kwa awamu zote na tusubirie na kile kipande cha Morogoro, mwaka huu mtapanda treni.Fedha zipo wakati wowote mwaka huu kwa Dar- Moro kipande kile kitakamilika.

“Wanasiasa  kusema wanatimiza historia ya kukosoa kama mmoja tulivyomuona anakosoa ndege, lakini anakuja kupanda hiyo hiyo.Sisi hatutasita kuendelea kuchapa kazi.

“Licha ya kelele mbalimbali, nipo hapa kuwathibitishia miradi mingi ukiwamo wa  reli tunatekeleza kipande cha Dar – Moro, japo kinasumbua sumbua tupo vizuri kwa asilimia 75.

Alisema kipande cha Morogoro – Makutupora- Singida,  kimekamilika kwa asilimia 28, huku changamoto zikiwa ni mvua zinaendelea kunyesha kuwazuia mafundi kuendelea na kazi.

Alisema mpaka sasa wametumia Sh trilioni 2.957 kwa ajili ya mradi huo, ambapo alidai gharama ya mradi wote ni Sh trilioni 7.

Alisema leo makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, wanatarajia kuanza ziara ya kukagua mradi wa SGR.

“Hakuna kilichosimama wala  hakuna ‘tashtiti’ yoyote na kuanzia kesho (leo) tutakuwa na ziara muhimu ya kihistoria kwa makatibu wakuu kukagua mradi huo,”alisema.

Kuhusiana na watu wanaobeza miradi ya Serikali, alisema wao wanaendelea kuchapa kazi na siku moja watakuja kuitumia miradi hiyo hiyo.

“Siku wakiumwa  tutawatibu, siku wakitaka kupanda ndege tutawakatia tiketi,sisi ni kuchapa kazi tu,”alisema.

Alisema Tanzania imekuwa nchi ya 21 duniani kuweka mazingira na kuchagiza biashara ndogondogo.

Alisema kwa Afrika, ni ya nne na kwa Afrika Mashariki imekuwa ni ya kwanza.

“Wenzetu wanatambua  juhudi tunazofanya, kuna ripoti imetoka kuhusu Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 21 duniani kwa  kuweka mazingira na kuchagiza biashara ndogondogo kwa kupunguza kero mbalimbali,”alisema.

Alisema mpaka sasa Serikali imetoa Sh trilioni 1.275 kwa ajili ya  mradi wa kufufua umeme wa Rufiji ambapo gharama za mradi wote ni Sh trilioni 6.5.

“Kazi nyingi zinaendelea kwenye mradi huu, sio ndoto na kazi inaendelea, Tunaendelea na utekelezaji,”alisema.

Alisema Serikali ya Tanzania imetengeneza   chelezo kubwa katika Ziwa Victoria na mpaka sasa imetoa Sh bilioni 32 kwa ajili ya mradi huo.

Mwisho

Hatutagiza nguzo za umeme nje-Majaliwa

Na Amina Omari,Tanga

SERIKALI  imesema haitaagiza nguzo za umeme nje ya nchi kwa sababu wazalishaji wa ndani wamezalisha za kutosha.

Kauli hiyo, imetolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alipozindua kiwanda cha kuzalisha nguzo za umeme Muha Traders kilichopo Pongwe.

Alisema wakati wa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Serikali itatumia nguzo ambazo zinazolishwa  nchini.

“Tunanguzo nyingi,hatuagizi kutoka nje kwani zamani Serikali ilikuwa inapata hasara kuagiza nguzo nje ya nchi,”alisema Waziri Mkuu.

Aliwataka watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuhakikisha wanawasimamia kwa ukaribu wakandarasi wanaosimamia miradi ya REA ili kuhakikisha wanafanyakazi kwa ufanisi.

Alisema nia ya Serikali, ni kufikisha umeme maeneo yote ya vijijini na vitongoji ili kutoa fursa kwa wananchi kuitumia huduma hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alisema Serikali imepata Sh milioni  45 kutokana na kodi ya mazao ya nguzo.

“Baada ya agizo ulilolitoa la kukusanya kodi katika viwanda vya uzalishaji wa  nguzo, tumebaini deni la Sh milioni 162, tumewekeana utaratibu wa kulipa na mwekezaji,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles