23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Ujenzi hospitali ya Muhas wakamilika

Daktari bingwa wa tiba za dharura wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk. Andrew Sawe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) vitanda vya kisasa kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu viliyopo kwenye hospitali hiyo iliyopo Kibamba Mloganzila jijini Dar es Salaam inatarajiwa kuanza kazi Januari mwakani.
Daktari bingwa wa tiba za dharura wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Dk. Andrew Sawe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) vitanda vya kisasa kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu viliyopo kwenye hospitali hiyo iliyopo Kibamba Mloganzila jijini Dar es Salaam inatarajiwa kuanza kazi Januari mwakani.

NA GABRIEL MUSHI, DAR ES SALAAM

HATIMAYE ujenzi wa hospitali ya Chuo Kikuu cha Sayansi Muhimbili (Muhas) Kampasi ya Mloganzila, umemalizika Agosti 31 mwaka huu, na inatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Januari mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kutembelea eneo hilo, Makamo Mkuu wa Muhas, Profesa Ephata Kaaya, alisema chuo hicho sasa kinatarajia kudahili wanafunzi 15,000.

Profesa Kaaya alisema hospitali hiyo ni maalumu kwa kufundishia wataalamu wa masuala ya afya lakini pia itatoa huduma kwa wagonjwa wa aina mbalimbali zaidi ya 1,000.

Alisema hospitali hiyo ina uwezo wa kulaza wagonjwa 571 pamoja na vyumba vya upasuaji 13.

“Ujenzi wa hospitali hii unatokana na juhudi za Serikali baada ya kupatiwa mkopo wa riba nafuu na Serikali ya Korea Kusini uliosainiwa mwaka 2010. Mkopo huu wa kwanza wenye thamani ya dola za Marekani milioni 49.5, ulikuwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya kufundishia na kutolea huduma tu.

“Mwaka 2011, mkopo mwingine wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 27, ulisainiwa kati ya Serikali hizi mbili kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa pamoja na mifumo ya Tehama katika hospitali hii. Pia Serikali ya Tanzania iliongeza kiasi cha Dola za Marekani milioni 18, hivyo kufanya jumla ya gharama za ujenzi wa mradi huu kuwa Dola za Marekani milioni 94.5 (Sh bilioni 206.7),” alisema.

Alisema mkopo huo unatarajiwa kulipwa taratibu kwa kipindi cha miaka 40 kuanzia sasa.

Alisema hospitali hiyo ikianza kutumika, itapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wagonjwa na gharama kubwa zinazotumika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya magonjwa kama vile figo na moyo.

Aidha, alisema pamoja na ujenzi wa jengo la hospitali hiyo lenye ghorofa tisa, utafuatiwa na majengo mengine kwa ajili ya makazi ya wafanyakazi na jengo maalumu la wagonjwa wa moyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles