25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Ujenzi daraja la mto Gide kuanza kujengwa rasmi

Brighiter Masaki

Ujenzi wa daraja la mto Gide kuanza kujengwa jumatatu baada ya wananchi kupata shida ya kupita kwa muda wa miaka 10.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkandarasi anaetarajia kujenga daraja hilo Nevablack Mwakalinga amesema kuwa wanatarajia kuanza ujenzi huwo rasmi siku ya Jumatatu.

“Tunatarajia kuanza ujenzi Jumatatu na tumepewa muda wa miezi mitatu lakini tunatarajia kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili kama mvua haitanyesha kwa wingi.”

“Daraja litakuwa na urefu wa mita kumi na moja na litakuwa la njia mbili ambalo lita ghalimu kiasi cha milioni 321 litakalo weza kupitisha magari ya uzito wa tani kumi pamoja na njia ya watembea kwa miguu” anasema Mwakalinga.

Kwa upande wa Diwani wa Kimara Baruti, Pasco Manota, anasema Halmashauri imetoa sh milioni 200, na Wakala wa barabara, TARURA imetoa malioni 100 kwaajili ya mchango wa ujenzi wa daraja hilo la mto Gide.

“Mkandarasi anatakiwa atoe kazi kwa wananchi wa eneo la baruti na makoka asipewe mtu wa kutoka mbali na eneo hili la ujenzi wa daraja ili lijenge kwa wakati.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles