22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ujenzi bwawa la Nyerer wafikia asilimi 67, kazi usiku na mchana

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati 2,115 umefikia asilimia 67.

Makamba alieleza hayo juzi, mbele ya wajumbe wa bodi ya Tanesco, wahariri na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa waziri Makamba, moja ya sababu za mafanikio haya ni ujenzi kufanyika usiku na mchana, jambo ambalo limeongeza kasi kwa kiwango kikubwa.

“Kasi kubwa ya ujenzi inaendelea katika mradi huu. Sasa hivi kazi inafanyika saa 24 usiku na mchana. Mtakuwa mashahidi leo (juzi) sikukuu ya Nanenane lakini watu wapo kazini na wanabadilisha zamu tu,” alisema Makamba.
 
Sababu nyingine aliyoelezea Waziri Makamba ni maboresho na mabadiliko yaliyofanyika katika menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na bodi yake ambazo zimekuwa zikifuatilia ujenzi wa bwawa hili na kuwasimamia makandarasi kwa ukaribu.
 
Akifafanua hatua hii iliyofikiwa, Waziri Makamba alisema “Ukitazama maendeleo ya mradi, miaka miwili na nusu ya mwanzo toka Disemba 2018 mpaka Juni 2021, tulifikia asilimia 37.
Leo tuko asilimia 67 (ongezeko la takriban mara mbili chini ya mwaka mmoja). Ni kasi kubwa katika kipindi kifupi,” amesema Makamba.

Katika ziara hiyo, wahariri na wanahabari walipata fursa ya kujionea maeneo nane muhimu katika mradi huo ikiwemo ujenzi wa tuta kuu (main dam) ambalo Juni 2021 ulikuwa asilimia 26 lakini hadi  hivi sasa asimilia 78.  Daraja la kudumu (permanent bridge) ambalo ni muhimu kupitisha vifaa vya ujenzi vyenye uzito mkubwa, ujenzi wake Juni 2021 ulikuwa asilimia 37.8, hivi sasa asilimia 95.
 
Pia, walijionea njia za maji kuendesha mitambo (power water ways) ambazo ujenzi wake kuanzia  Juni 2021 ulikuwa asilimia 43 sasa hivi upo 85. Jengo la mitambo (power house) Juni 2021 lilikuwa asilimia 29, sasa asilimia  51. Kituo cha kusafirishia umeme (switchyard) hadi Juni 2021 kilikuwa asilimia 38, sasa hivi asilimia 89.7.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles