28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘Ujasiri wa kukopa ndio utakaoboresha biashara, maisha yako’  

Mobil bezahlenNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TAKWIMU zinaonesha kuwa Watanzania wengi hawaendi kukopa benki licha ya kuwapo kwa fursa hiyo.

Sote tunafahamu kuwa benki ni wafanyabiashara kama walivyo wengine, wanauza na kununua fedha hivyo hiyo ndiyo bidhaa yao wanayoitegemea.

Hivyo, kama ni wafanyabiashara wanachotazamia ni kupata faida kama ilivyo kwa wengine. Kukopesha ni huduma wanayotoa kati ya huduma zingine nyingi walizo nazo na hivyo lazima kupata faida.

Sababu kubwa inayotajwa na watu ambao hawapendi kukopa benki ni kwamba wanadai masharti yao ni magumu, kuogopa kufilisiwa mali, riba kubwa na mlolongo mrefu wa kufuata taratibu ambazo zitamuwezesha mtu kukidhi vigezo vya kupata mkopo.

Wengine wanasema biashara zao si za kijasiriamali hivyo zinauwezekano mkubwa wa kufa hatimaye kushindwa kulipa deni.

Lakini pia, wengine wamekuwa wakikurupuka kukopa bila kupanga mipango madhubuti ya jinsi ya kurudisha – watu wanakopa ili kutatua matatizo yanayowakabili na si kuendeleza biashara zao.

Kwa kutambua umuhimu wa mikopo kwa Watanzania, kampuni mbalimbali za simu nchini zimebuni njia ya kuwakopesha wateja wao fedha taslimu kupitia simu zao za mkononi.

Tigo ni miongoni mwa kampuni hizo, ambapo inatoa mikopo kwa wateja wake papo kwa hapo bila vikwazo ili mradi tu uwe mtumiaji wa Tigopesa.

Mkuu wa huduma za Pesa kwa njia ya Simu wa Tigo, Raun Swanepoel, anasema kwa mara ya kwanza huduma hiyo iliyopewa jina la Tigo Nivushe itawawezesha wateja wa Tigopesa  kujiwekea historia ya  kukopa na ambayo inakuwa wazi kwa mteja yeyote na kuachana na aina nyingine za  ukopeshaji.

Hakuna dhamana inayowekwa au kuchukuliwa kwa kuwa huduma hii imeanzishwa ili iwe wazi na kuwezesha ukopeshaji kistaarabu.

Akifafanua kuhusu urahisi wa  huduma yenyewe, Swanepoel anasema Tigo Nivushe inatoa vipindi tofauti vya ukopeshaji zikiwamo gharama  tofauti za utawala  kulingana na urefu wa kukaa na mkopo.

Anatoa mfano mkopo wa wastani wa Sh 10,000 hufanyiwa kazi ndani ya muda mfupi  na fedha huingizwa kwenye akaunti ya mhusika ndani ya  dakika chache.

“Wateja waliojiwekea historia ya kukopa wanaweza kukopa kiwango  kikubwa cha fedha na ada ya uendeshaji ikiwa ni ndogo. “Mikopo hutolewa  moja kwa moja kwenye  pochi ya simu hivyo wateja  wanaweza mara moja  kutumia fedha hizo kulipia ankara (bili), kuhamisha  kwenda kwa wengine  au kuchukukua fedha taslimu kutoka kwa maelfu ya mawakala waliopo nchini.

“Tigo Nivushe imetengenezwa katika namna  ambayo inatoa msukumo wa ukopaji wa kuwajibika. Awali  mtindo wa simu uliokuwapo ulitumika kupima  ukomo mzuri wa mikopo na wateja  waliweza kuwa na mkopo mmoja kwa wakati.

Ulinzi dhidi ya mitikisiko ya kimaisha umejumuishwa ambapo kila mmoja atakayepata mkopo atajumuishwa moja kwa moja na atapewa bima dhidi ya kifo au ulemavu wa kudumu,” anasema na kuongeza kuwa ujasiri wa kukopa ndio utakaoboresha biashara au maisha ya mkopaji, ili mradi tu awe na desturi ya kurejesha kwa muda unaotakiwa.

Anasema muhimu zaidi ni kwamba kwa kuwa  bidhaa hii ina ada ndani yake, hakuna riba itakayolimbikizwa kwa tukio la kushindwa kulipa au kuchukua mkopo  hakuwezi kuathiri simu au akaunti ya Tigopesa kwa namna yoyote ile,” anasema Swanepoel

Mkuu huyo wa Huduma za fedha anaendelea kusema; “tunayo furaha leo kuzindua Tigo Nivushe. Ni bidhaa muhimu katika kuendesha shughuli jumuishi za kifedha ambao ni muhimu kwa Tanzania katika  kuendelea kukuza na kufanikisha uchumi wake. Mikopo hii midogo inaweza kuleta mabadiliko na ni muhimu katika kujenga  historia ya kukopa na kupata mikopo hapo baadaye.”

Huduma za fedha kielektroniki zilizo na usumbufu zilizokuwa zinatolewa na simu za mkononi tayari zimeshabadilisha maisha ya  mamilioni ya watu. Pamoja na huduma hii mpya ya kukopa kistaarabu, Tigo inataka kubadilisha  namna ambavyo watu wanafikiri kuhusu kukopa ikiwamo kuwaondolea woga walioujenga kuhusu mikopo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles