29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘Uingizaji vitu haramu magerezani uliishtua wizara’

Na BENJAMIN MASESE-MWANZA

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amesema kasi ya uingizaji vitu haramu na biashara ndani ya magereza nchini, uliishtua wizara hiyo na kuamua kuunda kamati ya kuchunguza mianya iliyokuwa ikitumika kutekeleza hayo.

Alisema hivi sasa jambo hilo likijitokeza katika gereza lolote, hatua zitachukuliwa kuanzia kwa mkuu wa gereza na watumishi wengine watakaokuwa wamehusika au kuzembea kwa namna yoyote ile.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa akiwa  na uongozi wa Gereza la Butimba, Masauni alisema tayari kamati iliyoundwa imekamilisha kazi yake na kukabidhi taarifa na mapendekezo yake wizarani.

“Niseme mpaka sasa tatizo hilo limepungua na imani yetu litaisha kabisa, angalizo ni kwamba ikitokea gereza fulani kumetokea hali hiyo, makamanda na watumishi wengine watawajibika, wito wangu ni kuwataka kuwa wakali  kweli kweli, haiwezekani sehemu kama ile kukafanyika biashara haramu, wizara tumepokea mapendekezo na tumeanza kuyafanyia kazi,” alisema.

Masauni alimtaka Mkuu wa  Gereza  la Butimba, Hamza  Rajabu kumweleza anavyotekeleza sera ya Serikali ya viwanda ambapo alisema ndani ya gereza hilo kuna kiwanda cha ushonaji nguo na wamekuwa wakipata kazi mbalimbali kutoka mashirika ya umma na binafsi.

Licha ya kupewa majibu hayo, Masauni alisema alichogundua uongozi wa gereza hilo bado hauna mpango mkakati wa kuliwezesha kujitegemea kwa chakula licha ya uwepo na hekari 479 za kulima mazao mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mwanza.

Awali, Rajabu alimweleza Masauni kuwa gereza hilo limezidiwa na watu kwani uwezo wake ni kuchuchua wafungwa 934, lakini waliopo sasa ni  1,888.

Alisema magereza yote ndani ya mkoa huo yana uwezo wa kuchukua  watu  1,249 lakini waliopo ni 2,633.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles