UINGEREZA YAKUBALI KUONDOKA  KWA AWAMU UMOJA WA ULAYA

0
520

Brussels,  Ubelgiji


UINGEREZA imekubali mpango wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kujiondoa katika muungano huo kwa hatua.

Waziri wa Uingereza anayeongoza mpango huo, David Davis, amekubali kusimamisha mazungumzo kuhusu mikataba ya  biashara kati ya pande hizo mbili hadi hatma ya raia wa pande hizo walioko mataifa ya EU na fidia ya mwisho ya kujitoa kuafikiwa.

Amesema ni wazi pande zote mbili zinataka kupata mustakabali mzuri wa uhusiano wao.

Naye Mwakilishi wa EU katika mazungumzo hayo, Michel Barnier amesema  pande zote mbili zinaweza kufikia makubaliano ya haki  na ni bora zaidi kuliko kutofanya hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here