Brussels, Ubelgiji
UINGEREZA imekubali mpango wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kujiondoa katika muungano huo kwa hatua.
Waziri wa Uingereza anayeongoza mpango huo, David Davis, amekubali kusimamisha mazungumzo kuhusu mikataba ya biashara kati ya pande hizo mbili hadi hatma ya raia wa pande hizo walioko mataifa ya EU na fidia ya mwisho ya kujitoa kuafikiwa.
Amesema ni wazi pande zote mbili zinataka kupata mustakabali mzuri wa uhusiano wao.
Naye Mwakilishi wa EU katika mazungumzo hayo, Michel Barnier amesema pande zote mbili zinaweza kufikia makubaliano ya haki na ni bora zaidi kuliko kutofanya hivyo.